Mhandisi Abdel Aziz Salem, Mkuu wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika la Soka





Abdel Aziz Abdullah Salem, amezaliwa mwaka 1895, katika Kituo cha Abu Kabir ndani ya Mkoa wa Al-Sharkia, alikulia katika familia
yenye hadhi vijijini  vya Misri, elimu yake ya kwanza ilikuwa huko Zagazig, na baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari, alisoma katika kitivo cha Kilimo, alikuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya kitivo hicho, kisha aliendelea masomo yake katika chuo kikuu cha Uingereza cha Cambridge,  huko akawa mmoja wa timu ya Wapiga Makasia wa chuo kikuu hicho.




Mhandisi. Abdel Aziz, alirudi Misri pamoja na ndoto na mafanikio yake ili kuteuliwa katika Wizara ya Kilimo kwa muda wa miaka miwili, baadaye alihamia kufanya kazi katika Wizara ya Maarifa, lakini  miaka miwili baadaye aliamua kurufi kwa Wizara ya Kilimo ili kufanya kazi katika  Maslahi ya Mali ya Kifalme



Mhandisi. Salem, alipandisha cheo kama  wakala msaidizi  hadi alipostaafu, na mnamo kipindi hicho hicho, Mhandisi. Salem, alichaguliwa kuwa Naibu katika Baraza la Bunge kwa vipindi viwili.


Wakati wa Mapinduzi ya kimisri yalipoanza mnamo  Julai 23,1952 jina la mhandisi Abd El Aziz Abd Allah Salem lilirudi mara tena, alipoteuliwa waziri wa mambo ya ndani na vijijini katika Wizara ya Ali Maher Basha, hiyo ilikuwa kabla ya kuanzishwa kwa Wizara ya Kilimo, iliyoanzishwa na mapinduzi 1952, kisha akawa Waziri wa Vijijini katika serikali ya kwanza ya Misri baada ya mapinduzi ya Julai 1952,kisha akawa Waziri wa Kilimo Katika serikali ya kwanza mnamo Septemba 7 ya mwaka huo, Ikiongozwa na Jenerali Mohammed Nageeb

Katikati ya Oktoba , Salem alikutana na wakulima wakuu kueleza baadhi ya maswala yanayohusika kutekeleza sheria ya mageuzi, ikiwemo kupunguza kodi ya ardhi kwa mara saba ya ushuru ,ikiwa ardhi ni ndogo makubaliano yanaweza kufanywa kati ya mpangaji na mwenye nyumba kukodisha ardhi kwa pesa au kwa macho yake, akisisitizia kwamba mpangaji analazimisha kurutubisha na kutunza ardhi, na Sheria hii iliainisha maeneo ambayo ngano inapaswa kulimwa na kiasi chake nchini.
Alisisitiza umuhimu wa wakulima hao kuendelea kulima ardhi hii na kuitunza na serikali itakapoliteka itawalipa fidia kwa mujibu wa desturi iliyofuatiliwa huku akiwakumbusha ni kiasi gani walichokipata siku za nyuma hivyo, itakuwa na madhara gani ikiwa wangeacha baadhi ya faida zao kwa faida ya idadi kubwa ya watu wa taifa.

Mnamo Novemba 24, 1952, Mhandisi. Salem alihudhuria tafrija katika Klabu ya Maafisa wa Jeshi ili kuzungumzia Sheria ya Marekebisho ya Kilimo na athari zake kwa maisha ya Wamisri, akisisitiza kwamba uzalishaji wa kilimo hautaathiriwa na ugawaji wa ardhi kwa wakulima wadogo.

Mapema mwezi wa Disemba aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu uwaziri. Salem pia alishika wadhifa wa Mkuu wa Chama cha Wakulima katika kipindi cha uhai wake.
Mhandisi Abdel Aziz Abdullah Salem aliongoza Shirikisho la Misri, akimfuatia  Luteni Jenerali Muhammad Haidar Pasha, Waziri wa Vita. Alishika wadhifa huo kwa awamu tatu, ya kwanza mnamo Septemba 26, 1952 , ya pili (kuanzia Januari 15, 1954. hadi Agosti 31, 1956 ), na ya tatu (kuanzia Agosti 31, 1956 hadi Februari 11, 1958 ).

Wakati wa vikao hivi vitatu, Mhandisi Abdel Aziz Abdullah Salem alikuwa na uangalifu ya kuhudhuria mikutano ya Baraza Kuu la Shirikisho la Kimataifa huko Zurich, Uswizi. Na wakati wa mikutano ya FIFA mnamo 1954, Mhandisi Salem alidai haki ya Misri ya kuwa mjumbe wa Ofisi ya Kiufundi ya Shirikisho la Kimataifa na mara ya kwanza, ombi lake lilikataliwa vikali.

Mhandisi Abdel Aziz Salem alitishia kujiondoa,na tayari aliondoka kutoka kwa mkutano ila katibu wa FIFA ameshughulikia suala hilo na amwombe Mhandisi Abdel Aziz Salem arudi kwenye mkutano na kusikiliza mahitaji yake,na mara tu baada ya kurudi tena alipewa nafasi ya kuzungumza,na alizungumza mbele ya hadhira kwa  Kiingereza kwa ufasaha uliowashangaza washiriki,na kubadilisha taswira ya kiakili ya hadhira kuhusu mmisri wa zamani mwenye kofia nyekundu, na mwishoni mwa mkutano huo,Misri ilikubaliwa katika ofisi ya kiufundi ya Shirikisho la Kimataifa.

Mnamo Juni 1956,na pembezoni mwa  kufanyika mikutano ya FIFA Congress katika mji mkuu wa Ureno huko Lisbon; Mhandisi Abdel Aziz Salem, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Misri, Mohamed Latif, Youssef Mohamed kutoka Sudan, Abdel Rehim shadad,Badawi Mohamed na Abdel Halim Mohamed,na mwaafrika kusini  Willam Phill wamekutana Kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuanzisha Shirikisho la Soka la Afrika(Baraza linalosimamia Soka Barani Afrika) kwa msaada wa Rais Gamal Abdel Nasser.

Manamo Februari 8, 1957.wawakilishi wa Misri,Sudan,na Afrika kusini walikutana na wawakilishi wa Shirikisho la Ethiopia walijiunga nao katika Hoteli ya Grand katika mji mkuu wa Sudan huko Khartoum ,na rasimu ya sheria iliwekwa na kujadili upangaji wa toleo la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika.

Na baada ya kuidhinisha  vifungu vya mfumo wa kimsingi, Mmisri Abdulaziz Abdullah Salem alichguliwa kuwa Mkuu kwa wingi wa kura, kwa hivyo akawa Mkuu wa kwanza katika historia ya Shirikisho hilo.

Mnamo siku ya kumi ya mwezi huo huo wa Februari, na baada ya mkutano wa kwanza wa jumuiya wa Shirikisho hilo, Mji mkuu wa Sudan ulishuhudia mwanzo wa Kombe la Mataifa ya Afrika, na hiyo kwa matakwa ya Dkt. Abdulhalim Mohammed, Mkuu wa Shirikisho la Sudan kwa Mpira wa Miguu, na kwa heshima kwa jukumu lake katika uungaji wa mkono kwa mhandisi Salem na juhudi zake kubwa katika kuanzisha Shirikisho la Afrika. Na kwa wingi wa kura mashindano ya kwanza ya Kombe yalipewa jina la mhandisi Abdulaziz Salem kwa heshima kwa juhudi zake kwa kuwa mmoja wa wakuu wa Mpira wa Miguu wa kiafrika na mwenye sababu ya kwanza katika kuujitokeza kwenye uwanja wa kimataifa. Mhandisi Abdulaziz Salem alinunua Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mali yake kutoka Khan El-Khalili nchini Misri, na linafanana na kombe la Ligi ya Mabingwa ya Uingereza .


Na nchi tatu kutoka Bara la Afrika zilishindana, ambazo ni Misri, Ethiopia na Sudan mwaka wa 1957, na Misri ilishinda mashindano ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika, lakini haiwezi kulibaki Kombe hilo la thamani baada ya ushinda wa Ghana wa mashindano ya mara  tatu, ya mwisho yalikuwa mwaka wa 1972, na kulibaki kwake kwa Kombe hilo mileleni.

Na hiyo ilikuwa mwanzo wa safari yenye furaha,uhai na nyakati nyingi zisizoweza kusahaulika hadi leo na hatua zinazoelekea kufafanua sura na sifa za Soka la Afrika.

أخبار ذات صلة: