Majadiliano kuhusu maswala mbali mbali ya jamii ya kimisri kwa mahudhurio ya Rais ElSisi kwenye mkutano wa Vijana wa Kitaifa kesho
- 2019-07-29 16:13:56
Rais Abdel Fattah Al Sisi anafungua shughuli za mkutano wa Vijana wa
Kitaifa katika kikao chake cha saba katika mji mkuu mpya wa kiutawala
" Kesho Jumanne" 30/8/2019
chini ya kauli mbiu "buni na ondoka", ambapo kundi kubwa la vijana wa
Misri kutoka kwa mikoa tofauti wanashiriki katika majadiliano kuhusu maswala
muhimu zaidi ya Jamii ya kimisri.
Na kikao kitafanyika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Kitaifa wa
Vijana kuhusu mfano wa Uigaji wa nchi ya Misri, na siku ya pili ya kazi za
mkutano huo unashuhudia sherehe ya kuhitimu kwa Programu ya Rais ya Ukarabati
wa Vijana wa Kiafrika , Kama mkutano wa kwanza pia unashuhudia kufanya kwa
mpango wa "Maisha mazuri," na
kisha Rais ElSisi anajibu katika kikao cha (Muulize Rais) kwenye maswali ambayo
yanazunguka katika akili za vijana katika
nyanja mbali mbali za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Balozi Bassam Radhi msemaji rasmi wa Urais wa Jamhuri,alisisitizia
taarifa za waandishi wa habari siku ya (Jumapili 28/7/2019) kwamba vikao vya
vijana vya ndani na vya kimataifa, ambavyo serikali imekuwa na hamu ya kupanga
kwa miaka, kulingana na maagizo ya rais, vina viwango vya ndani na vya nje ,
kama fursa ya mazungumzo mazito na ya moja kwa moja kati ya Viongozi na vijana,
ambayo imefanya faida nyingi katika ngazi mbali mbali za kijamii, kisiasa,
utalii na kiuchumi.
Balozi Radi alisema kwamba "Ulinzi na kukaribisha wa Mkutano wa
Vijana wa Ulimwenguni Inathibitisha
uongozi wa Misiri na ulinzi wake wa maswala ya vijana" , Akieleza
kwamba wazo la Mkutano wa Kitaifa wa Vijana chini ya kauli mbiu ya "unda
na ondoka" ulioanzia Oktoba 2016 ulikuja kudhibitisha kwa ukubali wa
serikali kutoa fursa kwa vijana kuelezea matarajio yao na mahitaji na maswala
yao; Ambaye alifanya kuna hali ya pekee ambayo haikuonekana nchini Misri hapo
awali, Hali inaelezea mawasiliano na
uwazi kati ya vijana na serikali na ushiriki wa kundi kubwa la vijana wa miaka
tofauti, vikundi na utaalam kutoka mikoa tofauti.
Msemaji rasmi pia amesisitiza kwamba Rais AlSisi kuhudhuria na kushiriki
katika mikutano yote ya vijana kuanzia Mkutano wa Kwanza wa Vijana wa Kitaifa
uliofanyika Oktoba 2016, kupitia mikutano ifuatayo ya vijana iliyofanyika
katika mikoa tofauti ya Jamhuri na kusikilizia maoni ya vijana na kurekodi
mwenyewe na ungiliana nao, Ambayo imeendeleza sana jukumu la vijana Waligeuka
kutoka kwa wasikilizaji na wapokeaji wa matukio kwa wazungumzaji na wasemaji
ambao wanapatia maoni na mawazo yao moja kwa moja katika maswala na faili mbali
mabli kwa uhuru na kwa uwazi.
Radhi alifafanua kuwa mkutano huo pia ulikuwa fursa ya kuunda mazungumzo
ya jamii kati ya vikundi vya vijana wenyewe.Mikutano hiyo haikulenga tu masuala
ya kiuchumi au kisiasa, lakini pia ilijumuisha mambo mengine ya kijamii na
kibinadamu. Mikutano hiyo ilikuwa jukwaa la mazungumzo, ukumbi wa michezo ya
sanaa na vipaji na jukwaa la kuwania vijana waumbaji ,wabunifu na mabingwa
Katika nyanja zote na sekta za serikali, mkutano huo uligeuka kuwa muumbaji wa
roho chanya na matumaini kwa jumla.
Balozi Radhi alisema kwamba upangaji huu mzuri wa mikutano huu
unaonyesha uwezo wa nchi ya Misri kutunza vijana na ulinzi wa maoni yao ,
pamoja na kujadili maswala ambayo inachukua maoni ya umma katika ngazi za ndani
na za kimataifa. na alisema kwamba mikutano ya vijana ya ndani na ya kimataifa
inathibitisha kwamba Misri Kwa mujibu wa maono ya uongozi wake Inachukua na
kutafuta kuanzisha njia ya amani, kuacha ghasia, na kukataa ugaidi,
kushughulikia ubinadamu na kusisitiza wazo la kueneza utamaduni wa mazungumzo
na ushirikiano mzuri kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Comments