Waziri wa Vijana na shirika la " Confejes " wanatoa ruzuku kwa vijana wenye miradi midogo midogo.

Katika sehemu ya
ushirikiano wa kimataifa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na shirika la confejes,
linaloshirikiana na Shirika la Kimataifa la La Francophonie, Dkt Ashraf Sobhy,
Waziri wa Vijana na Michezo, alitoa udhamini kadhaa kwa vijana wenye biashara
ndogo ndogo. Ruzuku hizo ni sehemu ya programu ya kusaidia na kufadhili mradi,
ambayo hutekelezwa kila mwaka chini ya usimamizi wa Utawala Mkuu wa Uwezeshaji
Vijana kwa ushirikiano na shirika katika nchi wanachama.
Naibu Mkurugenzi wa
Programu za Vijana katika tasisi ya Confejes Bw.Ibrahim Boubaker Kalousi,
Mkaguzi wa Fedha wa tasisi Paul Joachim Vignino Godono na kutoka Wizara ya
Vijana na Michezo Meja Jenerali Ihab Al-Basheer Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt.Ashraf
Elbejriemi mkuu wa sekta ya michezo na bi. Manal Gamal wa Utawala Mkuu wa
Uwezeshaji Vijana wailihudhuria Hafla ya makabidhiano hayo.
Tukio hili linakuja
ndani ya mfumo wa Mpango wa Ufadhili wa Biashara Ndogo katika nchi wanachama wa
tasisi, ambao unalenga kusaidia na kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa ruzuku
za kifedha na kiufundi ili kuendeleza miradi yao, kuunda fursa za kazi
endelevu, na kuimarisha mchango wao kwa uchumi wa ndani na wa jamii.
Dkt Ashraf Sobhy,
Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika nguvu za
vijana, ambazo zinanufaisha jamii na nchi nzima. Alieleza kuwa ushirikiano wa
kimkakati kati ya Wizara na tasisi ya Confejes unalenga kuwawezesha vijana
kiuchumi na kukuza ujasiriamali kwa jamii.
Nchi ya Misri, chini
ya uongozi wa uongozi wa kisiasa, inaweka umuhimu mkubwa katika kutoa njia
halisi kwa vijana kufanya kazi, kuzalisha, na kuvumbua.
Waziri aliongeza kuwa
Wizara ya Vijana na Michezo inajitahidi kila wakati kufungua upeo mpya kwa kila
kijana mwenye ndoto anayotaka kuigeuza kuwa mradi wenye mafanikio. Ruzuku hizi
zinaonyesha maono ya taifa la Misri ya kujenga uchumi wa kimaendeleo ambapo
vijana wanashiriki kikamilifu na ni washirika katika maendeleo na kufanya
maamuzi.
Wajumbe hao wa Confejes
pia wameelezea kushukuru kwao kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Vijana na
Michezo, na kupongeza juhudi za Misri katika kutekeleza mipango endelevu
inayolenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza ubunifu na ujasiriamali ndani
ya dira iliyo wazi ya kujenga kizazi chenye tija na ushawishi katika jamii
yake.
Inakumbuka tasis ya Confejes,
iliyoanzishwa mwaka wa 1969, ni tawi la Shirika la Kimataifa la La
Francophonie. Inafanya kazi kusaidia serikali za nchi wanachama katika kuunda
na kutekeleza sera na mikakati inayohusiana na vijana na michezo. Kupitia
programu zake mbalimbali, inachangia kufadhili miradi midogomidogo na kusaidia
maendeleo ya vijana katika nchi za Kifaransa.