Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, azindua Jukwaa la Kitaifa la Michezo la Huduma za Kidijitali "Score"

Wakati wa juhudi za nchi za kuimarisha Dijitali katika sekta ya michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ameanzisha Jukwaa la kimichezo la kitaifa kwa huduma za kidijitali Score, ambalo limeundwa na kuwekwa katika programu na Idara Kuu ya Mifumo ya Habari na Mabadiliko ya Kidijitali ya Wizara hiyo. Jukwaa hili lilianzishwa kwenye hafla za maonyesho ya "Sports Expo 2025", ambayo ni moja ya hafla kubwa za michezo katika eneo hilo
Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Sobhy alisema kuwa jukwaa hili jipya linawakilisha hatua muhimu kuelekea kwenye mabadiliko ya kidijitali ya huduma za michezo nchini Misri, kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kutoa data muhimu za kidijitali kwa sekta ya michezo. Data hizi zinajumuisha habari kuhusu vilabu, vyuo vya michezo, vilabu vya afya, wanariadha waliosajiliwa, mashindano, makambi ya michezo, mafanikio ya taasisi za michezo, vilabu na vifaa vyake, na mengineyo. Pia, jukwaa hili litalenga kuhimiza uwekezaji katika sekta ya michezo na kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuwepo.
Dkt. Sobhy alibainisha kuwa mpango huu unakuja katika mfumo wa mkakati wa serikali wa mabadiliko ya kidijitali, na kwa kufuata maono ya Misri 2030, ambayo inalenga kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi na kuhamasisha ubunifu katika sekta ya michezo.
Alisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia katika kuendeleza miundombinu ya michezo na kuimarisha mawasiliano kati ya vyombo mbalimbali vinavyohusika na sekta hiyo.
Alisema kuwa jukwaa hili litasaidia kufanikisha malengo ya "Misri 2030" kwa kujenga sekta ya michezo iliyoendelea na endelevu, ambayo inasaidia maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha nafasi ya Misri katika ramani ya michezo ya kimataifa.
Aidha, Dkt. Sobhy aliongeza kuwa Jukwaa la Kitaifa la Michezo la Huduma za Kidijitali linafanya kazi kwa kuzingatia maoni ya Wizara ya Vijana na Michezo ya kujenga mustakabali bora wa michezo ya Misri, kwa kuzingatia misingi ya mkakati wa serikali wa maendeleo endelevu na maono ya Misri 2030 katika michezo, ambayo inalenga kufanya Misri kuwa kituo cha kimataifa cha michezo kupitia misingi mikuu kadhaa.