Waziri wa Vijana na Michezo afanya mkutano ili kufikia mahitaji yote ya uidhinishaji wa maabara ya kimisri ya kugundua Madawa ya kusisimua misuli


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alifanya mkutano kwa mahudhurio ya jenerali Dkt.Mohamed Saad Hegazy, mkurugenzi wa kusimamia huduma ya kitabibu ya vikosi vyenye silaha, Dkt. Hazim Hamis, Mkuu wa taasisi ya Misiri ya kupambana na Madawa ya Kusisimuamisuli, na jenerali Mohamed Badawy, Mkuu wa maabara ya kimisri ya kugundua Madawa ya Kusisimua misuli.
Mkutano ulitaja maelezo yote ya uidhinishaji wa mwisho wa maabara ya kimisri ya Madawa ya Kusisimuamisuli, kuonesha na kujadili vikwazo vyote.
Waziri alionesha kuwa uidhinishaji wa maabara ya kimisri utakuwa hatua muhimu ya kukuza udhibiti wa matumizi mabaya ya dawa za kusisimua misuli kati ya wachezaji, ndani ya mfumo wa ujali wa Misiri kuhakikisha uadilifu wa mashindano ya michezo.
Aliongeza:"tunafanya kazi kufikia vigezo vikubwa vya ubora vya kupambana na steroids na utafiti wa kisayansi, na hivyo kwa kuratibu na taasisi ya Misiri, kurahisisha vikwazo na kutosheleza njia zote za uimarishaji ili kupata uidhinishaji wa mwisho wa maabara kulingana na vigezo vya kimataifa, jambo ambalo litasaidia kukuza hadhi ya mchezo wa kimisri kwenye kimataifa"
Mkutano ulihudhuriwa pia na Dkt. Zakaria AlKhayat, Mkuu wa kitengo cha (I.c) kwenye taasisi ya kitaifa ya utafiti, Dk. Amany Abd El ghani, Mkuu wa kitengo cha ubora kwenye kitivo cha tiba ya Ain Shams, Dkt. Shimaa Al Tasbiti, mkurugenzi wa kiufundi wa maabara ya kugundua Madawa ya Kusisimua misuli kwenye taasisi ya kitaifa ya utafiti, na Dkt. Eman Gomaa, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Misiri ya kupambana na Madawa ya Kusisimua misuli.