البحث

Waziri wa Vijana na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki wawaheshimu mabingwa wa timu za taifa za Karate

2025/04/12


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Mhandisi. Yasser Idris, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, waliwaheshimu wachezaji wa timu za taifa za karate (vijana, wavulana,  wenye chini ya umri wa miaka 21), kwa mahudhurio ya Bw. Mohamed El Dahrawy, Rais wa Shirikisho la Karate la Misri, na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho. Hafla hiyo ilifanyika kwa kuthamini mafanikio makubwa ya wachezaji katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa, yaliyojumuisha Mashindano ya Dunia, Kombe la Dunia, na Ligi Kuu ya Dunia.


Sherehe ya heshima ilipongeza uchezaji bora wa kiufundi na kimwili wa wachezaji. Timu ya taifa ya vijana ilishinda medali tatu (mbili za dhahabu na moja ya shaba), timu ya taifa ya wavulana  wailishinda medali nne (dhahabu moja, mbili za fedha na shaba moja), na timu ya chini ya miaka 21 ilishinda medali sita (tatu za dhahabu, mbili za fedha na shaba moja).


Matokeo hayo yamesababisha wachezaji saba wa timu za taifa kufuzu kwa Michezo ya Dunia, itakayoandaliwa na China m,Agosti ijayo. Wachezaji hao ni pamoja na mchezaji mmoja wa kiume wa kata, wachezaji watatu wa kiume kumite, na wachezaji watatu wa kike wa kumite. Mafanikio haya yanaonesha kiwango cha maendeleo ya mfumo wa karate wa Misri na kuendelea kwake kutafuta viwango vya juu vya kimataifa.


Katika hotuba yake, Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa Wizara inaweka umuhimu mkubwa katika kusaidia mashirikisho ya michezo na kutoa huduma zote zinazowezekana kwa mabingwa wa Misri katika michezo mbalimbali. Alibainisha kuwa mafanikio ya mabingwa wa karate yanaakisi juhudi kubwa zinazofanywa katika mafunzo, maandalizi, na wafanyakazi wa kiufundi na wa utawala, na kuimarisha hali ya michezo ya Misri katika ngazi ya kimataifa.

Waziri huyo alibainisha kuwa kusaidia na kukuza vijana wenye hodari ni ndani ya mfumo wa dira ya taifa la Misri ya kujenga vizazi vya wanariadha wenye uwezo wa kushindana na kushinda michuano mikubwa. Alipongeza jukumu la Shirikisho la Karate la Misri katika kuandaa timu za taifa zenye uwezo wa kuwakilisha Misri kwa njia bora zaidi.


Alieleza kuwa Shirikisho la Kimataifa la Karate limekubali kuipa Misri Ubingwa wa Ligi ya Dunia 2026, jambo linalodhihirisha mafanikio ya Misri katika kuandaa mashindano mbalimbali, pamoja na kiwango cha juu kilichofikiwa na Shirikisho la Misri na wachezaji, na imani yao kwa Misri kuandaa michuano hiyo.


Waziri wa Michezo alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza kwamba wachezaji wa Misri sasa wameandika majina yao katika historia ya taekwondo ya Misri, na sasa wanachuana na Japan, mabingwa wa dunia katika mchezo huo.

Kwa upande wake, Mhandisi Yasser Idris, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, alisifu jukumu kubwa lililofanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirikisho la Karate na juhudi zote zilizofanywa kuendeleza karate ya Misri.


Alisisitiza kuwa Shirikisho la Karate ni miongoni mwa mashirikisho ya Misri yenye mafanikio makubwa kiutawala na kiufundi, hali inayodhihirika katika ushindi wake wa mataji na ubingwa, na pia katika mashindano yake ya michuano yote ambayo dunia nzima imekuja kusifia uchezaji wa wachezaji wa timu ya taifa.


Kwa upande wake, Mhe. Mohamed El Dahrawy, Rais wa Shirikisho la Karate la Misri amemshukuru Waziri wa Vijana na Michezo na Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Misri kwa ushirikiano wao katika kukuza maslahi ya taifa na kuendeleza michezo nchini Misri.


Akielezea kufurahishwa kwake na kiwango kilichofikiwa na wachezaji wa Misri, alisisitiza kuwa siku zote wamekuwa na wanaendelea kufanya kazi hiyo na hawaepukiki kutwaa mataji na kuinua jina la Misri katika majukwaa ya kimataifa.

أخبار ذات صلة: