Shule ya Majira ya Joto ya Kiafrika 2063

Ni mojawapo ya miradi ya Mpango wa maelewano ya Kiafrika katika toleo lake  la nne katika mfumo wa kambi ya kuelimisha inayolenga Viongozi Vijana wenye ushawishi kutoka mikoa ya Misri mbalimbali,wanafunzi wageni wa Afrika. shule inatoa masuala kadha ili kujadiliana kifikra baina ya vikundi vya vijana kwa nyanja za (Sayansi za Siasa / Uchumi / Anthropolojia / Historia / Jiografia / Urekebishaji wa Taasisi / Amani na Usalama / Vyombo vya Umoja wa Afrika / Kuunda Uwezo wa Kibinafsi).

Mpango wa shule hiyo unajumuisha ziara za hali halisi pamoja na warsha na mihadhara, kama vile kutambulisha Hati ya Vijana wa Afrika na njia za kupambana na Ufisadi miongoni mwa Maoni ya Misri ya 2030, na maoni ya Umoja wa Afrika kuhusu Ufisadi (kuanzia kuwa kauli mbiu inayoshikiliwa na Umoja wa Afrika  kwa mwaka 2018 ni kupambana na Ufisadi. ), mwishoni mwa Utafiti huo, wanafunzi hutoa mitazamo kuhusu  jinsi ya kutekeleza matarajio ya Ajenda ya Afrika 2063 na maoni  ya Misri ya 2030 katika  hali halisi kupitia miradi ya kweli.

Shule ya Majira ya Joto ya kiafrika ya 2063 inategemea Hati ya Vijana wa Afrika kama hati ya mwongozo.

Malengo ya Shule ya Afrika 2063:

1) Kuandaa  kada Vijana  wanaoamini kwa dhana ya Umoja wa Afrika.

2) Kutambulisha Hati ya Vijana wa Afrika.

3) Kujihusisha Vijana waafrika wasio Wamisri katika jamii ya kimisri.

4) kuunganisha  vizuri wakimbizi   kupitia elimu ya kuwasiliana . 

5) Kufafanua na kuunganisha Maoni ya Misri ya 2030 katika Kiwango cha kitaifa - Ajenda ya Afrika 2063 katika Barani - na malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 kimataifa  pamoja na maendeleo ndani ya bara la Afrika.

6) Kuimarisha viunganishi vya  kiutamaduni, kijamii na kihistoria kupitia elimu  kati  ya vijana wa nchi za Kiafrika.

7) Kutambulisha mchakato wa kukata maamuzi katika Umoja wa Afrika.

8) Kuweka mkakati wazi unaolenga kubadilisha itikadi ya watu wa Afrika kuhusu bara la Afrika.

-9) kuelimisha kwa  jukumu la mashirika na taasisi za bara la Afrika.

 10) kuelimisha  kwa Mtu mwafrika kutoka upande wa  kiutamaduni na kifasihi.

Inayohusiana na mada hii: