Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Mnamo Juni 1956, na pembezoni mwa  Mikutano ya FIFA Congress iliyofanyika  katika mji mkuu wa Ureno, Lisbon; Mhandisi Abdulaziz Salem, Mkuu wa Shirikisho la  Soka la Misri, Mohamed Latif na Youssef Mohamed, Bw. Abdel Rahim Shaddad kutoka Sudan, Badawi Mohamed, Dkt. Abdel Halim Mohamed, na mwafrika Kusini William Phil walikutana kuandaa mpango wa kuanzisha Shirikisho la Soka la Afrika. (Baraza kuu la Soka Barani Afrika).

Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya FIFA Congress mwaka 1954, huko Bern, Uswisi,  na ilipigwa kura kutambua Afrika kama Shirikisho la bara, na kulipatia bara hilo haki ya kumteua mwakilishi wake wa kwanza katika Kamati ya Utendaji, Abdel Aziz Abdullah Salem kutoka Misri.

Mnamo Februari 8, 1957, wawakilishi wa Misri, Sudan, na Afrika Kusini walikutana, na wawakilishi wa Shirikisho la Ethiopia walijiunga nao, kwenye Hoteli ya Grand katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na mswada wa sheria ulitayarishwa, na kuandaa toleo la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika lilijadiliwa.

Baada ya kuidhinisha kwa mswada wa sheria , Mmisri Abdel Aziz Abdullah Salem alichaguliwa kuwa Mkuu kwa kauli moja, hivyo kuwa Mkuu wa kwanza katika historia ya Shirikisho hilo.

Siku ya kumi ya mwezi huo wa Februari, na baada ya mkutano wa kwanza wa Baraza Kuu la Shirikisho, mji mkuu wa Sudan ulishuhudia kuzaliwa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, ambalo Misri ilishinda toleo lake la kwanza, na huo ukawa mwanzo wa tukio lililojaa furaha na uchangamfu na matukio mengi yasiyosahaulika hadi leo, na hatua katika njia ya kufafanua sura na sifa za Soka la Afrika.

Inayohusiana na mada hii: