Jopo la wakaguzi wa CAF, walifika mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu
wa 2019, limezindua ziara yake ya kwanza
ya ukaguzi kwenye viwanja
vitavyofanyikia mashindano (michuano) ya
Fainali ya kombe ya mataifa ya Afrika (AFCON)
yatakayopigwa nchini Misri,
kuanzia tarehe 15, mwezi wa
Juni hadi tarehe 13, mwezi wa Julai, mwaka 2019.
Ujumbe wa bodi ya uongozi ya shirikisho
la soka la Afrika CAF, unaongozwa na mwenyekiti wa michuano, Bw. Samson Adamu pamoja na
wenzake kutoka katika tume ya kitaifa
LOC, ulianza ziara yake kwa kutembelea
uwanja wa kimataifa wa jiji la cairo, kisha jopo hilo likatembelea uwanja wa Suez na uwanja wa Port said
na mwishoni mwa ziara yao walifika ulitembelea mjini Alexandria,
kwenye bahari ya kati-na-kati.
Miongoni mwa maeneo yaliofanyiwa ukaguzi
na jopo hilo kutoka katika makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu
(soka) barani Afrika lilifanya ukaguzi wa viwanja na makazi na usafiri na mawasiliano na mahospitali pamoja na ulinzi wenye amani na usalama nayo ni muhimu sana kwa upangiliaji bora wa
mzunguko wa 32 wa michuano iliyopambanuka barani Afrika itakayochezwa nchini Misri.
Comments