Taasisi ya KULINDA URITHI WETU chini ya ulezi wa waziri wa vijana na na michezo, mkutano wa kiarabu wa kiafrika wa urithi chini ya kauli mbiu ya "urithi ni tuzo ya raia"
- 2019-04-28 12:30:26
Taasisi ya KULINDA URITHI WETU chini ya ulezi
wa waziri wa vijana na na michezo, mkutano
wa kiarabu wa kiafrika wa urithi chini ya kauli mbiu ya "urithi ni
tuzo ya raia" na usimamizi wa mkuu wa ofisi kuu ya bunge na wa elimu ya
kiraia BI.Dina Fuad inandaa sherehe za siku ya kimataifa ya
urithi Jumanne,tarehe 30 Aprili katika
kituo cha elimu ya kiraia katika Aljaziira mjini Aswan ambao ni mji mkuu wa
vijana wa kiafrika .
Mkuu wa baraza la makatiba wakuu wa taasisi
Adel Munib amefafanua kuwa siku hiyo husherehekewa na mataifa mbali mbali
ulimwenguni kote tarehe 18 Aprili. Na
siku hiyo imeainishwa na baraza la kimatifa la majengo na maeneo ya
kiutamaduni (ICOMOS) ili kuisherehekea
kila mwaka. Na hayo yanatimia chini ya ulezi wa
shirika la UNESCO na shirika la
urithi wa kimataifa kwa ajili ya siku ya kimataifa ya kulinda urithi wa
kibindamu kulingana na makubaliano
yaliyopitishwa na mkutano mkuu wa shirika la umoja wa mataifa wa malezi,mafunzo na utamaduni mjini
Paris mwaka 1972.
Mratibu
wa mkutano na mkuu wa tume ya mawasiliano ya kiafrika BW.Mohamed
AL-Saeed amefafanua kuwa taasisi
hiyo itaiandaa sherehe kubwa sambamba na
siku ya kimataifa ya urithi kutokana
na mkutano wa kiarabu wa kiafrika wa
urithi unaojumuisha mfululizo wa vikao vya kiutamaduni vinavyohusiana na urithi wa kimisri wa kiarabu na kiafrika. Na kikao cha
kwanza kinajumuisha mazungumzo kuhusu
jaribio la Rwanda na jinsi ya kunufaika nalo na katika kikao hicho
anazungumza balozi wa Rwanda Saleh Habiman. Na kikao cha pili kinajumuisha mazungumzo
kuhusu kuwawezesha wanawake wa kiarabu na wa kiafrika na katika kikao hicho
wanazungumza mkuu wa baraza la
kiarabu la wanawake wafanyabiashara BI.Abir Asaam
na mkuu wa kamati kuu ya mahusiano ya kigeni ya umoja wa mwanamke wa sudani nchini
misri DK. Suad Fakir. Na kikao hicho kinaongozwa
na mwanahabari Dina Mohsen ukiongezea na
kikao cha tatu cha shule ya kiafrika ya
2030 na ambacho kinajumuisha
mazungumzo kuhusu mfano wa kuigwa wa kuvumiliana na kukutana
kwa ustaarabu na kuitambulisha shule hiyo kwa kuizingatia kuwa ni moja ya miradi ya mpango wa uzinduaji wa
kiafrika iliyokuwa inaunda kumbi ya kutamadunisha inayowalenga viongozi
vijana watendaji katika mikoa ya misri na wanafunzi wa kiafrika waliokuja
kwa ajili ya kuujua muono wa misri wa 2030 na jinsi ya agenda ya Afrika
ya 2030 kuchangamsha pamoja na waraka wa Afrika kama waraka wa
mwongozo.
VileVile
mkurugenzi wa mipango ya taasisi
Rasha Maghazi amefafanua uhudhuriaji
wa balozi wa uswisi na mke wake mjini
kairo ukiongezea na baadhi ya mabalozi wa kiafrika na wa kiarabu
na mabalozi wa mambo ya kigeni wa kimisri
pamoja na baadhi ya wanahabari , wasanii na wanariadha.
Ofisa maalumu wa tume ya mapokezi Bosi
Hassan amesema kwamba patapokelewa
wahudhuriaj kwa mavazi ya
kiutamaduni yanayoonesha ustaarabu
na utamaduni wa Nubia nchini
Misri kutokana na kundi la wavulana na wasichana walioshiriki
mkutanoni.
Na ofisa maalumu wa tume ya maonesho Sali Madani
amesema kwamba kutafanyika
maonesho kwa ajili ya kazi za sanaa na
za mikono zenye mwonjo wa
kiutamaduni kwa ajili ya kundi la wasanii na wabunifu wa baadhi ya mataifa yaliyoshiriki mkutanoni kama vile , Misri, Sudani, Eritria, Jibouti, Siria, Palestina, Moroko na Aljeria.
Aidhaa ofisa maalumu wa uratibu mkutanoni Rasha Hussein
amefafanua kuwa mmoja wa waliokirimiwa mkutanoni ni
Ahmed Adirisi mwenye fikra ya mwonjo wa kinubia katika vita vya mwaka 73 sambamba na
sikukuu ya ukombozi wa Sinai
katika angalizo kuu la kitaifa na
. Aidhaa amepewa zawadi ya nishani ya nyota ya kijeshi na raisi Abdal
Fatah EL-Sisi . Nishani hiyo inayopewa kwa maafisa wa vikosi vya jeshi kwa ajili ya mashindano yao katika mapambano.
VileVile DK. Suhair Abdal Kadr amepewa zawadi
ya nishani kwa maamuzi ya mchango wake mkubwa na kusaidia kwake katika uwanja wa wenye nguvu maalumu ambao imeandaliwa mizunguko miwili miongoni mwa
mizunguko yake chini ya ulezi wa raisi Abdal Fatah EL-Sisi.
Aidhaa
mbunifu wa mavazi wa sudani Abiir EL-Ansari amefichua
maandalizi yake ya mkusanyiko
mpya wa mavazi ambayo inatazamiwa
kupendekezwa katika mkutano wa kiarabu wa kiafrika wa urithi kwa lengo la kuitambulisha
dhana ya tamaduni mbali mbali
ukiongezea na kuimarisha mahusiano ya kimisri ya kiarabu ya kiafrika.
Na kama inavyojulikana, Abiir EL-Ansari ni mmoja wa wabunifu wa mavazi wa sudani ambaye ameingia ulimwengu wa mavazi na umaridadi wa kisasa
tangu mwaka 2007 . Na mnamo miaka hii
ametoa mikusanyiko mbali mbali ya mavazi katika mataifa mbali mbali
ulimwengiuni kote. Na miongoni mwa mataifa haya ni Marekani, Saudi na kairo.
Comments