Shirikisho la karate linampa Rais Abd Alfatah Elsisi lakabu la michuano ya dunia
- 2019-10-30 17:14:14
Shirikisho la karate chini ya uongozi wa Mohamed Aldahrawy limeamua kumpa Rais Abd Alfatah Elsisi, rais wa jamhuri, lakabu la michuano ya dunia ambayo timu za kitaifa za vijana na vijana chini ya miaka 21 zimelishinda.
Misri imeshinda michuano ya dunia iliyofanyika nchini Chile, baada ya
kufuzu kwa medali 19 mbalimbali ambazo ni : medali 7 za kidhahabu, medali 4 za
kifedha na medali 8 za shaba.
Ukurasa rasmi wa shirikisho umetangaza uamuzi wa shirikisho, ambapo
katika ukurasa huu umeandika kuwa baraza la uongozi wa shirikisho la Kimisri Ia
karate chini ya uongozi wa Mohamed Aldahrawy, mwenyekiti wa shirikisho la
Kimisri Ia karate na baraza lake zuri linampa Rais Abd Alfatah Elsisi Ushindi
wa Misri kwa nafasi ya kwanza ya michuano ya dunia kwa vijana na vijana chini
ya miaka 21 iliyofanyika nchini Chile 2019.
Orodha ya wachezaji walioshinda medali ni : Basmla Hassan, Taha Tarek,
Yasmin Goweli, Ahmed Ayman, Hazem Ahmed na Ferial Ashraf na medali ya dhahabu
ya kata ya pamoja ya vijana katika mashindano ya timu, kwenye kiwango cha
medali za kidhahabu.
Na kwenye kiwango cha medali za kifedha : Mohamed Hussen, Fatma Abd
Anlasser, Hossam Mokhtar na timu ya wasichana katika mashindano ya timu.
Huku kwenye kiwango cha medali za shaba : Momen Mohamed, Abdallah
Hisham, Abdallah Mamdouh, Mahmoud Gaber, Nour Ehab, Youssef Badawi, Kareem
Waleed na Ahlam Youssef.
Imepangwa kuwa ujumbe wa timu ya kitaifa utarudi Misri kesho kutwa,
Jumatano, baada ya kushinda medali za kidhahabu, kifedha na shaba kutoka
mataifa 86 yaliyoshiriki katika michuano hiyo.
Comments