Ziara za uchunguzi ya kimisri kwa nchi za Kiafrika kutekeleza mpango wa "matibabu ya Waafrika milioni"
- 2019-11-01 13:28:51
Mhandisi "Aysem Salah "mshauri wa waziri wa teknolojia ya habari alisisitiza kuwa : Wizara ya Afya itatuma timu ya matibabu kwa nchi zingine za Kiafrika mwezi ujao kukagua na kubaini hospitali hizo ambapo hatua ya Rais Abdel Fattah El-Sisi itatekelezwa kuwatibu Waafrika milioni moja.Salah alieleza kuwa Kuratibu na nchi kabla ya kuanza kwa mpango huo kupitia matembezi ya uchunguzi ya timu ambayo huchagua hospitali inayofaa kwa utekelezaji wa mpango huo, na alibaini kuwa bado kuna utitiri mkubwa wa raia wa nchi za Chad na Sudan Kusini kwa mpango wa Rais ya kuwatibu Waafrika milioni moja, akisema kuwa serikali itatoa msaada wote kwa ndugu Katika nchi za Kiafrika zilizochaguliwa kutekeleza mpango huo, baada ya viongozi wa kisiasa kuelezea nia yao ya kuhamisha uzoefu wa mpango wa afya wa milioni 100 uliozinduliwa nchini Misri ili kuondoa virusi C, na kugunduliwa kwa magonjwa yasiyoenezwa , kwa nchi za Kiafrika, na akiashiria kuwa raia watasajiliwa Wakati wa mpango mpya wa mfumo, uliozinduliwa na Wizara ya Afya kusaidia nchi za Kiafrika katika kufanya uchunguzi, ni tofauti na mfumo wa mpango wa afya wa milioni 100 na hutegemea usajili wa raia na nambari za kitambulisho, kwani hakuna jumla ya taarifa kwa raia katika nchi za Afrika au sensa au takwimu makini ya Jumla ya raia.
Comments