Misri na Liberia zinacheza mechi ya kirafiki uwanjani mwa (Borg Alarab), siku ya 7 ya mwezi wa Novemba

 Mkurugenzi wa timu ya kitaifa ya kwanza, kocha Mohamed Barakat ametangaza  itifaki ya mwisho iliyofanyika kati ya shirikisho la soka la Kimisri na shirikisho la soka la Liberia ili kucheza mechi ya kirafiki kati ya timu mbili za kitaifa hizo, siku ya 7 ya mwezi wa Novemba ujao.

 

Na mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya kitaifa, kocha Hossam Albadry ameomba kucheza  mechi ya kirafiki mnamo siku ya 7 ya mwezi wa Novemba kwa ajili ya uandaaji wa wachezaji wa kitaifa aliyewachagua hivi karibuni katika njia ya uandaaji ili kuanzisha njia ya fainali iliyofikia kombe la mataifa ya Kiafrika 2021 nchini Cameron.

Timu ya kitaifa inakuwa tayari ili kucheza mechi mbili za Kenya na Visiwa vya Komoro, siku mbili za 14 na 18, mwezi wa Novemba ujao katika mraba wa fainali zinazofikia kombe la mataifa ya Kiafrika nchini Cameron.

 

Mkurugenzi wa timu ya kitaifa amesema kuwa mechi ya Liberia itacheza  kwenye Uwanja wa (Borg Alarab) mjini Aleskandaria , akiashiria kuwa timu ya kitaifa ya Liberia ni timu ya kitaifa inayopatikana mnamo wakati huu ili kucheza pamoja timu ya kitaifa ya Misri, huku timu zote za kitaifa zingine zinajali kwa matayarisho ya kucheza mechi katika fainali iliyofikia kombe la Afrika.

Timu ya kitaifa ya Misri imecheza mara nne dhidi ya timu ya kitaifa ya Liberia, mechi hizo zote zimekuwa katika fainali za kombe la dunia, ambapo timu ya kitaifa ya Misri imeshinda katika mara mbili, kwa  (2-0) katika fainali za kombe la dunia 1990, na ushindi mwengine kwa  (5-0) katika fainali za kombe la dunia 1998.

Huku timu yetu ya kitaifa imeshindwa mara mbili kwa tija hiyo hiyo (1-0).

Comments