Misri ilipata nafasi ya 19 kimataifa katika kikao cha michezo ya kijeshi nchini Uchina

 Tija za kikao cha michezo ya Kijeshi Ulimwenguni, kilichofanyika mjini Wuhan nchini Uchina, Kwa ushiriki wa wachezaji 10,000 kutoka nchi wanachama zaidi ya 100 wa Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Kijeshi, ambapo Misri ilipata nafasi ya  19 Baada ya kuzishinda medali 9 tofauti.

 wakati wa mashindano  yaliyodumu kutoka Oktoba hii 15 hadi 27, Misri ilishinda medali mbili za dhahabu kwa wachezaji: Mohamed Ibrahim El Sayed (katika Mweleka wa Kirumi uzito wa kilo 67), Islam Mahmoud Hamed na mchezaji Salma Ayman (katika Khomasi ya kisasa ya wawili).

 

Pia Nour Ahmed Hussein katika Taikondo, Mohammed Salah Al-Orabi katika Ndondi alifanikiwa kupata medali mbili za fedha, wakati mwengine  walishinda medali 5 za shaba na wao ni: Abdul Rahman Wael Abu Al-Khair, Saif Issa, Hedaya Malik katika Taekwondo na Abdul Latif Manea kwenye Mweleka wa Kirumi na Salma Ayman katika Khomasi ya kisasa.

 

Inataja kuwa wachezaji wa taasisi ya kijeshi wamepata mafanikio mengi katika kipindi cha mwisho, na wamechangia kuinua bendera ya Misri juu katika viwanja vyote vya michezo vya kikanda na kimataifa.

 

Ujumbe huo ulirudi nyumbani Kwenye ndege za kitaifa( EgyptAir), mdhamana rasmi wa ujumbe wa timu za kitaifa ya Misri.

Comments