Waziri wa vijana na michezo anashuhudia hitimisho la michuano mbili za kidunia za Skwashi kwa wanawake na Misri ya kimataifa
- 2019-11-06 12:28:12
Katika hitimisho la Kimisri Ia michuano mbili za skwoshi,
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, jioni ya jana, Ijumaa
ameshuhudia mwisho wa mashindano ya michuano mbili za kidunia za skwoshi kwa
wanawake, na michuano ya Kimisri ya kimataifa iliyofungwa kwa wanaume ambayo
imekaribishwa kwa Misri katika eneo la piramidi mkoani Giza.
Nour Alsherbeeny aliyeainishwa kama mchezaji wa pili
ulimwenguni amewezesha kufuzu kwa lakabu ya michuano ya dunia ya wanawake dhidi
ya Raneem Alwalily aliyeainishwa kama mchezaji wa kwanza ulimwenguni, kwa tija
3/1 na hiyo kwa mara ya nne katika historia ya Nour, huku Karim Abd Algawad
aliyeainishwa kama mchezaji wa nne ulimwenguni ameshinda lakabu ya michuano ya
Misri ya kimataifa ya wanaume dhidi ya Ali Farag aliyeainishwa kama mchezaji wa
kwanza ulimwenguni, kwa tija ya vipindi vitatu.
Imetajwa kuwa jumla ya tuzo za michuano ya wanawake
zimefikia dola elfu 430, huku tuzo za michuano ya wanaume zimefikia dola elfu
185.
Kwa upande wake, Waziri wa vijana na michezo amesisitiza
furaha ya kubwa kuwa wachezaji wa Kimisri ni wachezaji wa kwanza wa mchezo wa
Skwashi ulimwenguni.
Pia ametangaza kuwa wizara imekwisha vitendo vyote na
maandalizi yanayohusiana na uzinduzi wa mradi wa kitaifa kwa wavulana wenye
talanta ya Skwashi kwa umri wa miaka kuanzia miaka 6 hadi miaka 8 kwa uratibu
na shirikisho la Kimisri Ia Skwashi.
Na awamu ya kwanza ya mradi huo inajumuisha uangalizi wa wachezaji
250 ili kuanza mazoezi yao na uandaaji wao wa kiufundi, mwili na afya katika
kituo cha vijana cha Algaziera na eneo la michezo mjini port said kama awamu ya
kwanza imeanzia mwezi wa Desemba ujao.
Kisha awamu ya pili itakayoteklezwa katika vituo vya
maendeleo ya kimichezo katika eneo la Shubra Alkhaima na Sheraton, baadaye
mradi huo itakayoteklezwa mkoani mbalimbali ya Kimisri ili wanaohitimu kutoka
mradi huo kuwa msingi wa timu za kitaifa za Kimisri kuanzia umri wa miaka 14,
na hii ili kudhamini kwa kuendelea kwa
uongozi wa Kimisri wa kimataifa kwenye ngazi ya kushinda mashindano au kwenye
ngazi ya kukaribisha michuano, ukiongezea na uenezaji wa mchezo kati ya idadi
kubwa ya wavulana na vijana katika mikoa mbalimbali ya Kimisri.
lazima kutaja kuwa sherehe ya hitimisho imehudhuriwa na
idadi kubwa ya mashabiki pamoja na mahudhurio ya watu maarufu na wahusika
maarufu wa riadha, kisanii na pia wataalamu wa vyombo vya habari vya kimisri.
Comments