Maandalizi makubwa ili kuwakaribisha Maraisi wa nchi za bara la Afrika katika sherehe ya ufunguzi wa kombe la mataifa la Afrika

Kamati ya shughulu za sherehe inayoongozwa na Dkt. Tareq Kamal, ilianza kujiandaa kwa ajili ya sherehe ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa la Afrika, ambao utafanyika katika uwanja wa Kairo , 21 Juni ujao.

Tariq Kamal alisisitiza kuwa kamati inafanya mikutano nyingi ili kuandaa mpango wa kuwapokea wageni na wageni wakuu (VIP ) katika sherehe ya ufunguzi, hasa kwamba sherehe itashuhudia kuhudhuria  kundi kubwa la Maraisi na viongozi wa nchi zinazoshirika katika mashindano hayo.

Raisi wa Kamati ya shughuli za sherehe  alieleza kuwa Kamati inajadili mpango wa kuwakaribisha wageni na wageni wakuu (VIP ), Ili kuionyesha  sherehe kwa njia sahihi na kuendelea mafanikio yaliyopatikana wakati wa sherehe ya kupiga kura, ambayo iliwavutia wageni wa Misri, yakiwa kimaandalizi au kiuongozi.

Kamal alihitimisha maneno yake kwa kuashiria kwamba mpango wa shughuli za kuwakaribisha wageni wakuu inajumuisha waheshimiwa wengi ikiwa ni pamoja na Marais na mawaziri wa nchi zinazoshirikisha pamoja na marais wa vyama vya kiraia na wanachama wa kamati mbili za utendaji wa shirikisho la soak la kiafrika na Shirikisho la soak la kimataifa.

Comments