Kwa njia rasmi, Misri inapokea urais wa Mtandao wa kiafrika kwa Taasisi za kitaifa ya Haki za Binadamu
- 2019-11-06 13:25:01
Rais wa Baraza la Kitaifa kwa Haki za Binadamu Mohamed Fayek, alitangaza upokeaji rasmi wa Misri kwa urais wa Mtandao au mkusanyiko wa kifrika kwa Taasisi za kitaifa ya Haki za Binadamu kuanzia Jana Jumatatu, ambalo ni shirika la kikanda linalojumuisha taasisi za kitaifa ili kukuza na kulinda haki za binadamu barani mwa Afrika.
Hii ilikuja pembezoni mwa mkutano wa kumi na mbili wa
Mtandao wa Taasisi za kimataifa kwa Haki za Binadamu za Kiafrika, ambayo
matukio yake yalianza leo, katika Kairo
na kwa siku mbili, kwa mahudhurio ya
wakilishi wa nchi za kiafrika 44 wanachama wa kamati, na wakilishi wa
upande za kitaifa, kikanda na kimataifa zilizotunzia haki za Binadamu,na ujumbe
wa kidiplomasia.
Fayek alitangaza katika taarifa kwa Chombo cha Habari cha
Mashariki ya Kati kwamba mkutano huo wa Mtandao wa kiafrika kwa Taasisi za
kitaifa ya Haki za Binadamu ni tukio la kwanza kupangwa mjini Kairo
kama sifa ya Misri ni rais wa kisasa wa mtandao, akisisitiza kwamba
dhamira ya mkutano inazunguka kuhusu (Mkataba wa kimataifa kwa ajili ya
Uhamiaji: maoni ya pamoja kwa taasisi za kitaifa ya haki za binadamu na Fursa
na changamoto katika utekelezaji wake) .
Aliongeza kuwa suala la uhamiaji ni moja wapo ya masuala
muhimu zaidi yanayosabibisha wasiwasi
kwa mamilioni ya watu wa Kiafrika na ulimwengu ,Akisisitiza kwamba majadiliano
katika mkutano huo yanazingatia njia za utekelezaji wa maafikiano ya kidunia
kwa ajili ya uhamiaji salama na kwa utaratibu.
Inatajwa kwamba Misri ilitia saini hati ya kuanzisha Mtandao
wa kiafrika kwa Taasisi za kitaifa ya Haki za Binadamu kwenye hafla ya Mkutano
wa Sita wa Taasisi za kitaifa ya kiafrika kwa Haki za Binadamu, iliyofanyika
katika mji mkuu wa Rwanda Kigali mnamo
Oktoba 2007 na unaongozwa jijini Nairobi, nchini Kenya.
Maoni ya Mtandao huu au mkusanyiko yanalenga
kuhakikisha juhudi kwa kila nchi katika bara la Afrika iwe kuwa na taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu ya
kiutendaji , kwa kufuata kanuni za Paris na mchango katika kukuza haki za
binadamu na haki kwa raia wote wa bara la kiafrika.
Comments