Leo, waziri wa Vijana na Michezo anafungua Mkutano wa kiafrika wa 30 wa Tiba ya kimichezo chini ya kichwa cha "Changamoto na mapya katika Tiba ya kimichezo"


Dkt Ashraf Subhi, Waziri wa Vijana na Michezo na Dkt Constantine Rowe, Rais wa Umoja wa kiafrika wa Tiba ya Michezo, walifungua Mkutano wa kiafrika wa 30 wa Tiba ya kimchezo  chini ya kichwa cha "Changamoto na Mapya ya Tiba ya kimichezo" ulioandaliwa kwa Umoja wa Kiafrika wa Tiba ya kimichezo chini ya Wizara ya Vijana na Michezo na kwa kushirikiana na idara kuu ya Tiba ya kimichezo kwenye Wizara.

Ambapo Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza juu ya uangalifu wa wizara kwa  mikutano kama ile, kulingana na mwelekeo mkuu  mnamo awamu ya  sasa

Ni kuboresha tiba ya kimichezo , kushughulisha kwa kuboresha mfumo wa matibabu na wachezaji  ili kuepuka hatari ya majeruhi, ambayo yanaweza kuwanyima Misri na wachezaji wake kuwa mshirikishi  katika Michuano  na vikao vya kimataifa.

Na katika mkutano huu kundi jema la madaktari watatoa mhadhara ambapo, Dkt. Ahmed Abdel Aziz, ambaye anatoa mhadhara kwa anwani ya   (majeraha  ya goti na malalmiko ya misuli), Dkt Mamdouh Mahfouz  atatoa mhadhara kwa anwani ya (kusoma na taarifa"Ripoti" katika radiolojia ya kiuchunguzi), Dkt. Mohamed Kadri Bakri atatoa mhadhara kwa anwani ya  "Uandaaji wa kimwili na majeruhi" Dokta.  "Muhamed ElAraby Shamuon" atatoa mhadhara kwa anwani ya "physiolojia ya saikolojia (elimu ya nafsi ) ya kukabiliana na majeraha ya kimichezo" na Dkt Safaa Tawfiq al - Husseini (lishe bora ya wanariadha).

Mkutano ulihudhuriwa na Dkt Imad El Banani, Rais wa Shirikisho la kimisri na kiarabu  kwa spoti Wote, Dkt Mohamed Sobhi Hassanein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Umoja la Michezo la kimisri kwa Vyuo Vikuu na Dkt Hanan Abdel Moneim, Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Aswan.

Comments