Vijana na Michezo " Sebule ya Afrika" inakaribisha ujumbe wa wanachama wa Bunge ya Uganda

Wizara ya Vijana na Michezo , Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia , na Ofisi ya Vijana ya Afrika inakaribisha ujumbe wa wabunge wa Uganda wanaowakilisha utaratibu wakati wa shughuli za Sebule ya Afrika, kwa kushirikiana na Wizara ya Upangaji , Ufuatiliaji na Mageuzi ya Tawala, Taasisi ya kitaifa kwa Usimamizi . kwa ajili ya kutafutia njia za kuhamisha jaribio kuu la kimisri katika nyanja za kupanga, utawala na uwezeshaji wa vijana, na hayo yatatokea mnamo saa saa tisa mchana kwenye ukumbi wa mikutano kwenye ghorofa ya pili, Diwani Kuu ya Wizara.

Hii inakuja wakati wa urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika mnamo 2019 na katika mfumo wa juhudi za kitaifa za kidiplomasia zinazotolewa kwa ajili ya kuunda nyanja za ushirikiano na shughuli za pamoja kati ya nchi za Afrika.

Ujumbe huo ni pamoja na Dokta Albert Bemojisha, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Kitaifa , Mjumbe wa Bunge Henry Mussazi, Richard Sewakrienga, Mjumbe wa Baraza la Utawala la Kitaifa, Amos Golubi, Mjumbe wa Baraza la Utawala la Kitaifa, Dokta Tom Gedido, Mratibu wa Sekretarieti wa Meya ya Upimaji wa wakuu , na Bibi Judith Egang.

lengo la mkutano huo ni kutekleza diplomasia laini ya kufanya matembezi ya pamoja ili kusambaza uzoefu wenye mafanikio na kujadili matumizi yake kwa mifumo mengine iliyo na sifa zinazofanana ili kuunga mkono ufanisi wa utawala nchini Uganda kwa kuchunguza jukumu la vijana na jinsi ya kuwaunganisha na kuwahusisha katika mchakato wa kuamua na kwaelekea uongozi na mabadiliko kwa kushughulikia mada hiyo. kupitia kuangalia yaliyoteklezwa na wanafunzi waliopata mafunzo katika Wizara ya Vijana na Michezo kutokana na programu tofauti , na kuangalia tija na mapendekezo yake, pamoja na kuzingatia njia bora zaidi za kuboresha Mfumo wa Mapitio ya rika za Afrika, unaohusisha kwa mfumo wa utawala wa Uganda.

Comments