Vijana na Michezo hujadili njia za kuhamisha uzoefu mkuu wa kimisri katika nyanja za upangaji, utawala na uwezeshaji wa vijana kwenye "Sebule ya Afrika
- 2019-11-07 21:05:11
Wizara ya Vijana na Michezo "Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia na Ofisi ya Vijana ya Kiafrika" ilikaribisha mkutano wa wajumbe wa Bunge la Uganda wakiwakilishi utaratibu wa uhakiki wa rika ndani ya shughuli za Sebule ya Afrika, kwa kushirikiana na Wizara ya Upangaji , Ufuatiliaji na Marekebisho ya kiutawala. Sehemu za mipango, utawala na uwezeshaji wa vijana, kwa kuzingatia kuwepo kwa urais wa umoja wa kiafrika mnamo 2019 na ndani ya mfumo wa juhudi za kidiplomasia za kitaifa zinazotolewa kwa ajili ya kuunda nyanja za ushirikiano na shughuli za pamoja kati ya nchi za Afrika.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Albert Bemojisha, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Kitaifa na Mjumbe wa Bunge Henry Mussazi, Richard Sewakrienga, Mjumbe wa Baraza la Utawala la Kitaifa, Amos Golubi, Mjumbe wa Baraza la Utawala la Kitaifa, Dokta Tom Gedodu, Mratibu wa Sekretarieti wa utaratibu wa wakuu , na Bibi Judith Egang. Ghazali, Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Vijana ya Afrika, Makamu wa Rais wa Umoja wa kiafrika na Amira Sayed ni mwandishi wa habari kwenye gazeti El egyptian Gazet..
Youssef Wardani, Waziri Msaidizi wa Vijana na Michezo kwa Maendeleo ya Vijana, alielezea utaratibu wa wizara hiyo na serikali ya kimisri kwa uwezeshaji wa vijana, akizungumzia mpango wa rais kuwaelekeza vijana wa Kiafrika kwa uongozi na mpango wa urais wa kuwezesha vijana na ushirikiano wa pamoja kati ya wizara na chuo kufikia mkutano wa Vijana wa Ulimwenguni.
Kadriya Talha, Mkurugenzi Mkuu wa elimu ya kiraia na viongozi Vijana katika Wizara ya Vijana, alijadili shughuli za Idara Kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia, muundo na programu zake, pia jukumu la Shule ya Kiafrika katika kujenga viongozi wachanga, akitangaza matayarisho ya Programu ya kujitolea ya AU " Umoja wa kiafrika" kama mpango mkubwa zaidi wa kujitolea utekelezwe. mwishoni mwa mwezi huu.
Katika muktadha huu, Nelly Zein El Abidine, Mkurugenzi Mkuu wa Bunge, alielezea jukumu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika kama udhamini wa kwanza wa Kiafrika-Kiafrika katika kutoa mafunzo na kuwawezesha vijana waafrika unaosababisha kuchangia kujenga bara la Afrika kupitia juhudi za watoto wake, pamoja na kuangalia jukumu la Bunge la Vijana na wachanga . Itazinduliwa mnamo kipindi kijacho kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kairo na chini ya Uangalifu wa Waziri Mkuu.
Hassan Ghazali alianzisha kuonyesha Programu ya Wajitolea wa Umoja wa Afrika, wakati wa kukaribisha Kairo kwa mpango mnamo Desemba 2019, itakayofanyika Novemba na Desemba mwaka huu, na kutekelezwa na serikali ya kimisri kupitia Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Kameshina ya Umoja wa kiafrika nchini Ethiopia, akielezea utekelezaji wa mpango wa Ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Uganda ili kujenga uwezo wa viongozi vijana kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kuungana na kuimarisha ufanisi wa chombo cha kiutawala.
Heba Refai, mhadhiri katika Taasisi ya Mipango alieleza uzoefu wa shule hiyo ya kiafrika na jukumu lake katika utekelezaji wa mipango kama hiyo ya kuelimisha vijana na bara la Afrika, akisisitiza kwamba uzoefu wa kimisri unafanikiwa katika uwanja wa uwezeshaji na ujumuishaji wa vijana katika mchakato wa kufanya maamuzi , jinsi ya kuhakikisha Uwiano kati ya kuhakikisha maburidisho kwa vijana na kuzingatia shughuli za ujumla pamoja na kutekleza programu za kielimu, kiutamaduni na kimafunzo katika uwanja wa Uongozi.
wakati ambapo Ujumbe huo ulisifu jaribio kuu la Misri kwa kuwezesha wanawake na vijana kupitia kuwapa mafunzo katika uongozi.
lengo la mkutano huo ni kutekleza diplomasia laini katika ziara tofauti za pamoja ili kusambaza uzoefu uliofanikiwa na kujadili matumizi yao kwa mifumo mengine iliyo na sifa zinazofanana ili kuunga mkono ufanisi wa kiutawala nchini Uganda kwa kuchunguza jukumu la vijana na jinsi ya kuwaunganisha katika mchakato kuamua na kuwawezesha kwa uongozi na mabadiliko kupitia kuangalia shughuli tofauti zilizofanyika na wanafunzi wa Wizara ya vijana na michezo na kuangalia tija zake, pamoja na kuzingatia njia bora zaidi ili kuboresha chombo cha kiafrika kwa kuangalia wakuu , njia zinazohusisha kwa kuimarisha mfumo wa kiutawala nchini Uganda.
Comments