Mkutano wa kamati ya kimatibabu ili kukabiliana juu ya mpango kabla ya michuano ya mataifa ya Afrika

Mwenyekiti wa Kamati ya matibabu wa michuano ya mataifa ya Afrika chini ya miaka 23 inayopangwa kufanyika nchini Misri mnamo kipindi cha tarehe 8 hadi 32 Novemba, daktari Mohamed Soltan amekutana na makundi ya madaktari wanaofanya katika michuano hiyo ili kuweka mpango wa mwisho na kukabiliana juu ya njia ya kufanya kazi kabla ya masaa machache ya uzinduzi wa michuano hiyo.

Mohamed Soltan amesisitiza madaktari dharura ya kufuata maagizo ya Kamati ya utabibu, na kufanya juhudi zaidi wakati wa mechi na kutobadilika katika kazi ya utabibu wa kwanza ikiwa mchezaji yeyote ameumia na ikiwa wanachama wa matibabu wa timu ya kitaifa wanahitaji msaada wa makundi ya matibabu.

 

Pia amesisitizia madaktari kujali kwa mashabiki, hasa katika mechi za timu ya kitaifa ya Misri itakayohudhuriwa na idadi kubwa za mashabiki.

 

Imetajwa kuwa mechi ya kuanza itachezwa leo kati ya timu ya kitaifa ya Misri ya Olimpiki na mwenzake timu ya kitaifa ya Mali.

Timu za kitaifa 8 zitashiriki katika michuano, ambapo katika kila kundi lina timu 4  za kitaifa ,timu ya kitaifa ya Misri iko katika kundi la kwanza pamoja na timu za kitaifa za Mali, Cameron na Ghana, mechi za kundi hilo zitachezwa kwenye Uwanja wa kimataifa wa Kairo, huku kundi la pili linajumuisha Cote d'lvoire, Zambia, Nigeria na Afrika Kusini, mechi zao zitachezwa kwenye Uwanja wa mpira wa Salam.

 

Michuano ya mataifa ya Afrika itafikisha moja kwa moja timu zenye nafasi tatu za kwanza  kufikia Olimpiki ya Tokyo 2020.

Comments