Tangazo la Ofisi ya Vijana wa Afrika (kwa washiriki wasio wa Wamisri ) .... Nafasi ya kuhudhuria Mkutano wa 10 wa Vijana wa Kiafrika
- 2019-11-08 16:17:19
Mkutano wa 10 wa vijana waarabu na waafrika utafanyika mnamo 20- 26 Desemba 2019 (Kuwasili 19/12 hadi Kairo & Kuondoka 27/12 kutoka Kairo) huko Luxor na Aswan.
Tukio hilo limeandaliwa kwa Ofisi ya Vijana ya Afrika na Jumuiya ya Kiarabu kwa Vijana na Mazingira wakati wa Aswana ni Mji mkuu wa Vijana waafrika 2019.
Mshiriki atalipa tiketi na ada ya visa pia wakati waandaaji watalipa usafiri wa ndani, malazi, kujikimu na matembezi ya kitalii.
Maudhui za mkutano:
Urithi na majadiliano wa tamaduni.
Uwezeshaji wa vijana na wanawake.
Masuala ya vijana ya kimataifa kama " Ukosefu wa Ajira-
Uhamiaji Haramu- Ugaidi"
Masuala ya maji katika eneo la kiarabu na kiafrika.
Utoaji karatasi ya kiutafiti inayohusu maudhui yoyote ya
mkutano huo , utazidisha nafasi zako za kujiunga katika kikao kinachojadili
maudhui ile ile.
ukihudhuria Mkutano wa vijana wa dunia, utakuwa na nafasi ya kupanua makazi yako na kubadilisha tiketi ili kuhudhuria mkutano wa vijana waarabu na waafrika.
ukivutiwa kujiunga na kuhudhuria tafadhali ipeleke wasifu
wako kwa Email hiyo ([email protected]) kama dalili ya Uwezo wako wa kulipa
gharama za tiketi na Viza.
Comments