Timu ya kitaifa ya Misri inashinda timu ya kitaifa ya Mali kwa kufunga goli moja katika ufunguzi wa kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23

Timu ya kitaifa ya Misri imeshinda mwenzake timu ya kitaifa ya Mali kwa goli moja safi katika mechi iliyofanyika kati yao jioni ya leo, Ijumaa kwenye Uwanja wa mpira wa kimataifa wa Kairo, katika ufunguzi wa kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23 na litakalofikia Olimpiki ya Tokyo 2020, timu ya kitaifa ya Misri ya Olimpiki na mwenzake wa Mali ziko katika kundi la kwanza linalojumuisha timu za kitaifa za Ghana, Cameron, Misri na Mali. Timu za kitaifa 8 zinashiriki katika michuano hiyo zinazogawanyika kwa makundi mawili, na timu tatu za kwanza zitafikia Olimpiki ya Tokyo 2020. Kwa tija hiyo, timu ya kitaifa ya Misri imechukua nafasi ya kwanza kwa pointi 3, huku timu ya kitaifa ya Mali imechukua nafasi ya mwisho ya kundi hilo kwa pointi 0, na hii kwa kungoja kwa mechi ya Cameron dhidi ya Ghana itakayofanyika katika saa nne jioni ya leo ili kuainisha nafasi za kundi hilo baada ya awamu ya kwanza.

Comments