Siku ya
Jumatano (10 febuari 2019) raisi wa CAF amesema kwamba amemtembelea
kiupendo raisi wa Misri, EL-SISI katika
ikulu jijini kairo ili
kujadili kuandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya
kiafrika ukiongezea na mambo mengine.
Nakala ya 32 ya mashindano ya kombe la mataifa ya
kiafrika itafanyika kutoka 21 Juni hadi 19 Julai mwaka 2019 nchini Misri.
Katika mkutano huu
EL-SISI ametilia mkazo haja ya uratibu kwa vitendo
kati ya taasisi zinazohusika ili kudhamini
kufanikiwa kwa mashindano
haya kulingana na viwango vya
kikanda na vya kimataifa. Aidha, EL-SISI
amezitaka taasisi za serikali
kurahisisha kuboresha majengo na
miundombinu katika mataifa matano yanayohusiana na kuandaa
kwa mashindano hayo nayo ni
kairo, Alexendria, Ismailia, Suez na Port Said na khasa
mambo yanayohusiana na viwanja ,
shughuli za kiafya, uhamishaji pamoja
na mwawasiliano.
Baada ya kuchaguliwa kwake kuwa mkuu wa shirika la umoja wa kiafrika
katika kipindi cha kufanyika kwake kwa
kawaida kabla ya wiki kadhaa katika mji mkuu wa Ethiopia " Adis Ababa ", EL-SISI amesisitiza kwamba michezo na hasa mchezo wa
mpira wa miguu ina mchango muhimu wa
kueneza amani na muungano barani Afrika.
Na kwa upande wake raisi wa CAF
alimshukuru mwenzake wa
kimisri kwa kutilia umuhimu kwake kufanikiwa
kwa michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika inayoshuhudia ushiriki wa timu 24 kwa mara ya kwanza .
Na alimpa raisi wa Misri bendera ya
kumbukumbu. Akiashiria azma yake ya kupokea kuyaandaa mashindano na
akielezea mataraji yake kuwa kumbukumbu nzuri. waziri mkuu wa misri,
Mostafa Madbuli pamoja na waziri wa
vijana na michezo, Ashraf Sobhy wamehudhuria mkutano huu.
Comments