Waziri wa michezo anashuhudia. Hitimisho la mkutano wa pili wa vyombo vya habari kwa klabu ya kimataifa kwa vyombo vya habari vya kimchezo

 Dokta  Ashraf Sobhy waziri  wa  vijana  na  michezo  alishuhudia  siku  ya  Jumamosi  jioni kituoni  mwa  elimu ya  kiraia kwenye Al Gazira   , hitimisho  la  shughuli  za  mkutano  wa pili wa  vyombo  vya  habari kwa  klabu ya kimataifa  kwa vyombo  vya  habari  vya  michezo unaofanyiwa  chini  ya  usimamizi  wa  Waziri  wa  vijana  na  michezo  tangu  tarehe  7 mpaka tarehe  10 Mwezi  huu  wa  Novemba  .

 

Katika  mkutano  Waandishi wa habari  na wataalamu  wa  vyombo vya habari Waarabu  kadhaa waliuhudhuria,  na  programu yake  inakusanya   idadi  ya  mihadhara  na  mazoezi  ya  vitendo  ili  kujadili  vipengele  kadhaa  vinavyohusiana  na  kumwezesha mwenye vyombo vya habari bora , vyombo vya habari vya dijiti  , uratibu  wa  vyombo vya habari na  jinsi ya kuwa mtangazaji  bora  .

 

wanashiriki  wote  wa mkutano  wa  vyombo vya habari kwa  klabu  ya kimataifa  ya vyombo vya habari ya  kimichezo walisisitiza  uundaji  mkono  wa  Misri  katika  vita  vyake  dhidi  ya  ugaidi , wakiashiria wakati  huo huo  kwa  mahusiano ya ndani  yanayounganisha  Misri na  nchi  za  Kiarabu  chini  ya  uongozi  wa  Mheshemiwa rais Abdelfatah  elsisi  rais  wa  Jamhuri  .

 

Hitimisho  la  mkutano   linahudhuriwa na   mwanahabari   wa  Baharini   " Mouhamed  Qasm  " mwenyekiti  na  mwundaji  wa  klabu  la  kimataifa  la  vyombo vya habari vya  michezo  ,  mwanahabari  " Ahmed  shuber  " Naibu  wa  mkurugenzi  wa  klabu  kwa  bara  la  Afrika  , na mwanahabari  wa  Tunisia   " Adnan  bn Murad  " naibu   wa  kwanza  kwa  mkurugenzi  wa  klabu   pamoja  na  mwanahabari   wa   Yordani " Salaeh Rashad " .

 

Na  katika  kauli zake   , Dokta  Ashraf  Sobhy alifafanua  kuwa   wizara  ya  vijana  na  michezo  haikujali juhudi  yoyote katika  kuendeleza  kazi  ya  michezo  na  kivijana,   akitoa  pongezi  kwa  washiriki  wote  kwa mafanikio  ya  mkutano   yanayozingatia  Ushirikiano  wa  kiarabu  wa  pamoja  wenye  lengo  imara  kwa  kuendeleza  sekta  ya  michezo  .

 Vilevile  , waziri  wa vijana  na  michezo  alieleza  matarajio yake  kwa  mafanikio  mazuri  kwa  wote  na  kupata  Maendeleo  , ustawi na  mafanikio  bora  kwa  nchi yetu  ya kiarabu  .

 

Mkurugenzi  mwanzishi wa  klabu ya kimataifa  ya vyombo vya habari ya  kimichezo alisema kwamba   : " tunajivunia  kwa  msaada  wote   unaotolewa  na  wizara  ya  vijana  na  michezo  ya  Misri  kwa  klabu  ya kimataifa  ya vyombo vya habari vya michezo  " akiashiria  mvuto mkubwa  wa  wanachama  wa  klabu  ili  kushirikisha  katika  shughuli  za  mkutano  baada  ya  kujua kuwepo   toleo lake  la  pili   nchini  Misri  .

 

Alifafanua  kuwa  klabu  ya kimataifa  ya vyombo vya habari vya  kimichezo  imeanzia  waandishi  wa  habari  na  wataalamu  wa  vyombo vya habari  500  na  sasa  idadi  ya  wanachama  wao  imefikia  wanachama  3687  kutoka  nchi  mbalimbali  , alibainisha  kuwa  klabu  itashuhudia   uchaguzi  wa  kwanza  kupitia  miezi  3 na  nafasi  itapatikana  mbele  ya  wanachama  wote  ili  kugombea   katika  vyeo  vya  klabu  .

 

Kwa  upande  wake  , mtangazaji  " Ahmed shuber  " alitoa  shukrani  na  heshima  kwa  Waziri  wa  vijana  na  michezo  kwa juhudi  zinazofanywa  ili  kufanikisha mkutano  wa  vyombo vya habari vya  kimichezo  katika  toleo lake  la  pili   na  kuitika  mambo  yote  yanayohusu maandalizi  ya  mkutano  .

 

 

Shuber  akiashiria kwa  mafanikio  ya  shughuli  za  mkutano unaofanyiwa  na klabu  ya kimataifa  ya vyombo vya habari vya  michezo  , vilevile  kwa  mahaba  na  mahusiano  mema yanayokutwa  na  washiriki Waarabu  wa  Misri  wakati  wa  ziara  yao.

Comments