Bwana Ghazali yupo kwenye jalada la gazeti la "Master Mind" la kiafrika.


 Mnamo sura ya 57, iliyotoa mwanga juu ya hatua za Ghazali kwa kichwa cha "Rudia Mfalme" tangu ukuaji wake, kisha maisha yake ya kazi, kufikia uanzishi wa ofisi ya vijana waafrika kwenye wizara ya vijana na michezo,  Picha ya mwanzishi wa ofisi ya vijana wa kiafrika bwana Hassan Ghazali yupo kwenye jalada la gazeti la "Master mind " lenye Upanuzi mkubwa kati ya vijana wa kiafrika. 


Na idadi imekusanya ukuaji wa Hassan Ghazali katika familia ya kimisri, yenye Utamaduni wa kinuba, na njia ya kuboresha mawazo yake kuhusu bara la Afrika, nayo imempa Mila kama: Heshima, Upendo, na Fahari kwa lolote la kiafrika, kufuatia uwanja wa kazi yake na upenzi wake wa kubadilisha jamii yake y kitaifa na kikanda, kulingana na Imani yake kwa kauli ya " Misri ni kijiji changu, Afrika ni nchi yangu",  ambapo anaamulia kujenga uwezo wa vijana wa kiafrika watakaojenga Afrika baadaye katika nyanja mbili za kijamii na kiuchumi. 


Na gazeti linaonyesha hatua zake za kimaisha, alianza toka shughuli zake pamoja na Jumuia ya kiafrika kwenye Zamalek amabyo ilikuwa mwanzo wake barani, pia ilikuwa ikiitwa toka wanadiplomasia na wanafunzi waafrika nchini Misri tangu uanzishi wake 1956 "Nyumba ya Afrika",  kisha mchango wake kwenye eneo kale la "Bulak Abo Elena" wa kuongeza Uelewa wa haki za kiuchumi na kijamii, kufikia kwa uanzishi wa ofisi ya vijana waafrika kwenye wizara ya vijana na michezo 2014,ili kuwa taasisi inayounganisha vijana waafrika nchini Misri na kuendelea mahusiano ya kiafrika, kupitia kufanyika Ushirikiano na utekelezaji wa Programu kwa bara pamoja na taasisi za kitaifa zinazohusika kwa vijana wa kiafrika na kuimarisha maadili ya kiafrika yaliyopatikana na baba waanzishi wa shirikisho la umoja wa kiafrika 1963.


Na katika wakati ule ule, sura hii ilikusanya hatua zake kama Naibu kwa umoja wa vijana waafrika kwa kaskazini mwa Afrika, pamoja na mradi wake wa kimafunzo "Mibegu"kwa elimu inayolenga kuwepo uongozi katika watoto ili; wawe wanaobadilisha jamii zao, kulingana na Imani yake kwamba, Elimu ni ufunguo wa maendeleo na mabadilishano kwenye jamii za kiafrika kwani; inatoa nafasi ya kujenga uwezo wa watoto na kusisitiza Maadili mazuri ndani yake. 


Na gazeti lilionyesha lengo la Ghazali nalo ni: awe mbadilishaji wa jamii kupitia kutosheleza masuluhisho maendelevu kwa changamoto za kijamii na kiuchumi, na kufanya harakati ya vijana Kwa Afrika zima, na kukuza kiwango cha Uelewa kuhusu Afrika kienyeji na kikanda.

Comments