Misri iko mbeleni mwa uainishaji wa kimataifa kwa shirikisho la kiulimwengu kwa karate

 Shirikisho la karate la kiulimwengu lilitangaza orodha kuu ya nchi wanachama kwenye shirikisho .

 

Misri ilipata nafasi ya kwanza kwenye uainishaji kwa pointi

49245 ikishinda Uturki iliyopata nafasi ya pili kwa pointi 49080 , Japan ilipata nafasi ya tatu kwa pointi 46815 , Ufaransa ilipata nafasi ya nne kwa pointi 33075 , na Italy ilipata nafasi ya tano kwa pointi 31230 .

 

Misri iliweza kuwa mbeleni mwa uainishaji wa kiulimwengu kutokana na matokeo yake kwenye michuano ya ulimwengu wa vijana chini miaka 21 , iliyofanyika mnamo 23 hadi 27 Oktoba mjini Santiago, Chile  .

 

Wakati ambapo Misri ilipata nafasi ya kwanza kwenye takwimu ya medali baada ya kupata medali 7 za dhahabu ,4 za fedha na 8 za shaba , medali 19 za aina mbalimbali kwa ujumla .

 

Timu ya Misri ilifaidika kutokuwepo kwa Japan kama nguvu kubwa sana kwenye mchezo wa karate , ambapo Japan iliomba msamaha ya kucheza kwenye mashindano ya ubingwa kwa sababu ya vurugu iliyotokea mjini Chile kabla ya kuzinduka Mondial kwa siku chache.

Comments