Waziri wa Michezo kwa haraka anaingilia katika shida ya timu ya kitaifa ya Kenya pamoja na hoteli ya makazi huko Aleskandaria
- 2019-11-15 13:06:38
Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, aliingilia kutatua mgogoro wa ujumbe wa timu ya kitaifa ya Kenya kutoka Hoteli ya makazi ya Aleskandaria kutokana na malipo ya gharama ya kukaa katika hoteli hiyo.
Kwa harakati
haraka na uwajibikaji, Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy,
alifanya mawasiliano ya haraka na ubalozi wa Kenya na balozi wa Kenya huko
Kairo kupata suluhisho la shida ya
misheni na hoteli ya makazi.
Waziri huyo
pia alielekeza wasimamizi wa Wizara ya Vijana na Michezo kwa haraka kuwasiliana
na maafisa wa Hoteli ya makazi kule Aleskandaria ili kutuliza hali na timu ya kitaifa ya
Kenya, na kushughulika utulivu na taaluma hadi mwisho wa shida iliyopo.
Hatua za kasi
za Dokta Sobhy zinakuja kwa sababu ya
kutishia kufukuzwa kwa hoteli ya makazi kufukuza timu ya kitaifa ya Kenya na
taarifa za Mkurugenzi Mtendaji wa Kenya Bari Otino, kwamba timu ya kitaifa ya
Kenya inatishiwa kufukuzwa kutoka hoteli ya makazi mnamo usiku ya leo huko Aleskandaria kwa sababu ya malipo ya gharama ya makazi,
akisisitiza kwamba ujumbe wa Kenya hauna pesa zinatosha kulipia gharama ya
makazi, hadi umalize mchezo.
Waziri wa
Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy , anataka kuondokana kwa vizuizi vyote
vya ujumbe wa timu ya kitaifa ya Kenya na timu nyingine kwa sababu ya uwepo wao
kwenye ardhi ya Misri, inayowakilisha
moyo hai wa Afrika, na kwa mchango wake na majukumu yake kwa matukio yote ya
michezo na hamu yake ya kutoka kwa shida na kuepuka kuongezeka kwa shida zozote
zinazovuruga hali za kisasa.
Inatarajiwa
kwamba shida hiyo itasuluhishwa baada ya masaa machache baada ya Waziri wa
Vijana na Michezo kuwasiliana na ubalozi wa Kenya na kuwaamuru maafisa wa
wizara kuwasiliana na hoteli ya makazi na kuwahutubia kutuliza hali na misheni
ya Kenya hadi utatuzi wa mambo ya mwisho.
Timu ya
kitaifa ya kwanza ya Misri itakutana na mwenzake wa Kenya saa kumi na mbili
jioni kesho Alhamisi katika mchezo wa kwanza wa kufikia Afrika
2021 nchini Cameroon.
Ni muhimu
kutaja kuwa Kundi la saba kufuzu kwa Mataifa ya Afrika 2021 nchini Cameroon ,
ni pamoja na: timu yetu ya kitaifa, Kenya, Tugo na Visiwa vya Komoro.
Comments