Waziri wa Michezo anaiunga mkono timu ya kitaifa ya Olimpiki dhidi ya Cameroon kwenye uwanja wa Kairo

 Waziri wa Vijana na Michezo Ashraf Sobhy  alikuwa na hamu ya kuhudhuria mechi ya timu ya kitaifa ya Misri na mwenzake wa Cameroon   miongoni mwa shughuli za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 23 ambayo  Misri itakayokaribishiwa mnamo kipindi cha Novemba 8 badi 22 .

 

 

Mechi hiyo ilihudhuriwa na mawaziri kadhaa, Amr El-Janaini ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya washiriki watano anayesimamia kutawala  Shirikisho la Soka la Misri kwa mpira wa miguu, Meja Jenerali Ahmed Nasser, mwenyekiti wa Shirikisho la mashirikisho ya Afrika, na maafisa kadhaa wa Shirikisho la Soka la Afrika kwa mpira wa miguu (CAF).

 

 

Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza uwezo wa wachezaji wa timu ya kitaifa ya Olimpiki kuendelea na utendaji bora, na kushinda michezo iliyobaki ya mashindano na kufikia Olimpiki ya Tokyo 2020, akielezea dhamira ya wachezaji kufurahisha watu wa Misri.

 

 

Waziri huyo aliashiria kuwa jukumu la hadhira wa Kimisri  waliokuwa na hamu ya kuja kwenye uwanja wa Kairo kuhamasisha na kuunga mkono timu ya Olimpiki, akionesha kutoa msaada wote kwa timu ya kitaifa na chombo cha kiufundi kwa uongozi wa  kocha Shawky Ghareeb.

Comments