ufunguzi wa michuano ya dunia ya kumi na nne pamoja na michuano ya Afrika ya kwanza kwa kuinua uzito kwa watu vipofu

ufunguzi wa michuano ya dunia ya kumi na nne pamoja na michuano ya Afrika ya kwanza kwa kuinua uzito kwa watu vipofu

 

 Jumapili, michuano ya dunia ya kumi na nne pamoja na michuano ya Afrika ya kwanza kwa kuinua uzito kwa watu vipofu zitaanza, zinazofanyika chini ya usimamizi wa wizara ya vijana na michezo mnamo kipindi cha tarehe 15 hadi 22, mwezi wa Novemba 2019 kwenye nyanja za hoteli ya (Cataract) katika eneo la piramidi saa kumi na mbili jioni.

 

Ufunguzi huo unashuhudia mahudhurio ya mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa ambaye ni (Nezam Dodol), Dokta Ahmed Mohamed Owin "mwenyekiti wa mashirikisho mawili ya Kimisri na Kiafrika' na wanachama wa kamati ya kimataifa ya kiufundi ambao ni : Dokta Hayat Khatab mwenyekiti wa kamati ya Kimisri ya Paralympics, wanachama wa baraza la shirikisho la michezo wa Kimisri kwa watu vipofu na wakurugenzi wa klabu zinazoshiriki katika shirikisho la michezo la watu vipofu.

 

Wachezaji 88 kutoka mataifa kumi wanashiriki katika michuano hiyo na mataifa hayo ni : Japan, Ukraine, Uhindi, Uturki, Urusi, Jamhuri ya Czech, Georgia, Venezuela na Libya pamoja na Misri iandaayo michuano hiyo.

Comments