Kamati iandaayo Mataifa ya Afrika inaandaa safari kwa vyombo vya habari vya nje kwa vivutio vya kale vya kidini

Kamati iandaayo Komble la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa 23 pamoja na idara ya utalii wa michezo kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, iliandaa safari kwa Msikiti wa Omar Bin El Aas na Mkusanyiko wa Dini. Na safari hiyo ilijumuisha wanahabari wote na vyombo vya habari vya nje nchini Misri ili kushughulikia mashindano hayo.

Ujumbe wa wanahabari hao uliambatana na Mohamed Khalil  mkurugenzi wa Idara ya Uelewa ya kiathari kwenye mikoa miwili Kairo  na Giza,Zinab Ebrahim  mkaguzi wa vitu vya kale kwenye Idara mkuu katika Kairo  na Giza na Ahmed Rafik  msimamizi wa Idara ya Utalii wa Michezo kwenye Wizara wa Vijana na Michezo.

Mzunguko huo umejumuisha ziara kwa Kanisa linalopachikwa linalojengwa marehemu karne ya tatu BK,iliyojumuisha alama 120 za bwana Kristo,Bikira Mary na watakatifu,pia Kanisa la Mtakatifu George ambaye mmoja wa watakatifu mashuhuri na pia alikuwa kiongozi wa Kirumi aliyeuawa alipoingia dini ya Ukristo,Kanisa la Abi Sarja, linalopata umaarufu wake kutokana na kuwa pango ambalo Familia Takatifu ilificha kwa miezi 3 na siku 15, pia Hekalu la Wayahudi la Ezra,ambayo moja ya masinagogi muhimu nchini Misri na ina vitabu vya hati na nyaraka muhimu kuhusu maisha ya Wayahudi nchini Misri na mzunguko huo ulihitimishwa kwa ziara ya Msikiti wa Amr bin Al-Aas ambao ni msikiti wa kwanza huko Misri na Afrika uliojengwa mwaka 641 BK .


Ujumbe wa wanahabari pia ulikuwa na hamu ya kununua makumbusho na kupiga picha pamoja na vivutio vya kihistoria, kuonyesha furaha yao kuwa nchini Misri na kutembelea vivutio vya kidini na kiutalii katika Misri ya kale na pamoja hiyo walitoa shukuru yao kwa kamati na Wizara ya Vijana na Michezo.

Na baada ya ziara hiyo, wizara ilihakikisha kuchukua ujumbe wa watu 40 kwenye safari ya Nile

Na mwishoni mwa mzunguko ujumbe wa wageni ulionyesha kufurahishwa na vivutio vya kale vya kimisri walivyotembelea na pia vivutio vya mji wa Kairo . Pamoja na walielezea shukuru yao kwa kamati na Waziri wa Vijana na Michezo kwa uangalifu wake kwa wageni.

Comments