Waziri wa vijana na michezo anaunga mkono wachezaji wa timu ya kitaifa ya Olimpiki kwenye mechi ya timu ya kitaifa ya Afrika Kusini
- 2019-11-20 23:15:06
Waziri wa vijana na michezo, Dokta Ashraf Sobhy amejali kwa uwepo katika chumba kikuu cha uwanja wa kimataifa wa Kairo ili kuunga mkono na kuhimiza kwa timu ya kitaifa Olimpiki ya mpira wa miguu katika mechi yake dhidi ya timu ya kitaifa ya Afrika Kusini katika nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Kiafrika chini ya miaka 23 inayokaribishwa kwa Misri.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Kiafrika (CAF), Ahmed
Ahmed na mwenyekiti wa kamati ya Khomasia
iliyoongoza Shirikisho la soka wamehudhuria mechi hiyo pamoja na idadi
ya maafisa.
Ushindi wa timu ya kitaifa ya Olimpiki ya mpira wa miguu
katika mechi hiyo, leo itaitoa Misri kadi ya kufikia Olimpiki ya Tokyo 2020,
ambapo inapangwa kuwa timu za kitaifa zenye nafasi tatu za kwanza katika
michuano hiyo zitafikia Olimpiki.
Waziri wa vijana na michezo ameashiria maonyesho
yaliyotolewa na wachezaji wa timu ya kitaifa ya Olimpiki katika awamu ya
makundi ya michuano hiyo na kuchukua nafasi ya kwanza ya kundi lao kwa pointi 9
ambazo wamezihakikisha kwa ushindi dhidi ya timu za kitaifa za Mali, Ghana na
Cameron, akielezea imani yake katika utendaji wa wachezaji na kujali kwao kwa
kuhakikisha ushindi na kufikia Olimpiki pamoja kuwafurahisha watu wamisri.
Waziri wa vijana na michezo ameyasifu mahudhurio ya mashabiki kwenye safu za viti
vya uwanja wa kimataifa wa Kairo ili
kuwahimiza wachezaji katika picha ya kistaarabu, ambayo ina athari kubwa kwa
kuwahimiza wachezaji ili kutoa utendaji bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha
ndoto ya kufikia Olimpiki.
Comments