"Ashraf Sobhy anampokeza bwana Soliman Musa Balozi mburundi mjini Kairo. "


Musa: Burundi imeichagua Misri kutokana na nchi tano (5) za kiafrika ili; kubadilishana ujuzi wa vijana pamoja. 

Sobhy: kuichagua Misri ni dalili ya mwelekeo sahihi ya nchi kwa maendeleo ya vijana. 


Mnamo mchana wa leo kwa tarehe ya 6, mwezi wa Mei, mwaka wa 2019 Dokta Ashraf Sobhy "waziri wa vijana na michezo " amempokeza Haji Soliman Musa "Balozi mburudani mjini Kairo "kwenye Diwani ya wizara. 


Bwana Sobhy amemkaribisha Balozi mburundi na alimpongeza kwa ujio wa mwezi wa Ramadhani takatifu, pia alimshukuru Balozi Soliman Musa kwa kuichagua Misri mshiriki  wake wa kutekleza Programu ya kubadilishana uzoefu wa vijana kati ya nchi hizi mbili, akisisitiza kwamba jambo hili linakuja kulingana na juhudi za nchi za kuwaboresha vijana na kuyabadilisha mawazo makale na kufuata njia mpya zinazoungana na hali ya sasa. 


Ameongeza kwamba mnamo mkutano wake na waziri mburundi wa vijana na michezo kwenye Sharm ElShekh, kulikuwepo mitazamo na maoni kadhaa zilizokabiliana nao. Pia upande wa kimisri unafurahi kwa kubadilishana uzoefu wa vijana pamoja na upande wa kiburundi. 


Na kwa upande wake, bwana Musa alieleza furaha yake ya kukutana na  bwana Sobhy, akisisitiza kwamba wizara ya vijana na michezo nchini Burundi pamoja na Programu ya maendeleo ya umoja wa mataifa, zote zinajali kutekleza Programu kwa kuwaboresha vijana na kubadilishana uzoefu pamoja na nchi nyingine za kiafrika. 

Ambapo nchi kadhaa za kiafrika zilichaguliwa nazo ni :"Misri - Kusini mwa Afrika - Morokoo- Tunisia- Senghal",  lakini Misri ndiyo iliyochaguliwa kwa wizara ya vijana na michezo pamoja na sanduku la umoja wa mataifa la kimaendeleo, kulingana na uzoefu mkubwa wa Misri, pia kipindi cha sasa Misri ina maendeleo makubwa ya vijana wamisri na kuwaelewesha. 

Kwa hiyo zote ziliwafikiana juu ya Misri, kwani; ina ujuzi mkubwa linalohakikisha mafanikio ya Programu na kuiboresha ili kupata faida kubwa kama inavyowezekana, na inayoamuliwa  kuanza Programu mnamo mwezi wa Juni ijayo. 


Mkutano huo ulihudhuriwa na Shaimaa Abo Abla" Msaidizi wa waziri kwa masuala ya kiafrika",  Reda Saleh" Mkurugenzi mkuu wa mahusiano ya kiujumla na ya nje",  na Ghada Hussen" Mkurugenzi mkuu wa mahusiano ya kimataifa ".

Comments