Kwa njia rasmi Misri inafikia olimpiki na inakabili Cote d'Ivoire katika mechi ya fainali ya mataifa ya Afrika

 Timu ya kitaifa ya olimpiki ilifanikiwa kuchukua kadi ya kufikia  olimpiki ya Tokyo 2020 na kufikia  mechi ya fainali ya mashindano ya  kombe la mataifa ya Afrika  chini ya miaka 23

Na hivyo ilikuja baada ya ushindi wa timu ya kitaifa ya Misri kwa Afrika kusini kwa mabao matatu , katika mechi iliyofanyika uwanjani mwa Kairo  na mashabiki elfu sabini waliihudhuria

 

Na Ramadan Sobhy  alifunga bao la kwanza kupitia penalti katika dakika ya hamsini na tisa kabla ya Abdelrahman Magdy alifunga bao la pili na la tatu kwa timu ya kitaifa ya Misri  mnamo dakika ya themanini na nne na ya themanini ya tisa kutoka mwanzo wa mechi.

 

Na inaamuliwa timu ya kitaifa ya kimisri ikutane na  Cote d'Ivoire katika mechi ya fainali ya mataifa ya Afrika na timu ya Ghana ikutane na mwenzake wa Afrika kusini ili kuchagua nafasi ya tatu na ya nne na kuamua timu gani  atakayekuwa mwenye  kadi ya tatu inayofikisha  olimpiki ya Tokyo.

 

Na Misri  inakaribisha mashindano yanayofikisha duru ya michezo ya kiolimpiki "Tokyo 2020" mnamo kipindi cha 8 hadi 22 katika mwezi wa Novemba  , ambapo wenye nafasi za tatu za juu wanaelekea moja kwa moja .

Comments