Wizara ya Vijana na Michezo inaandaa Tamasha la Kimataifa la watoto (kutoka miaka 12 hadi 17) mnamo kipindi cha Novemba hii 20 hadi 25 chini ya udhamini wa Waziri Mkuu Dokta Mostafa Madbouly. kwa ushiriki wa nchi 22 Wakati huo huo na sherehe za Umoja wa Mataifa kwa Siku ya watoto Duniani, iliyopitishwa mnamo Novemba kila mwaka, ambapo itashiriki Poland, Romania, Mexico, Sri Lanka, Indonesia, Yordani, Pakistan, Italia, Tunisia, Iraqi, Palestina, Uchina, Morocco, Siria, Ukraine, Ufaransa, Bangladesh, India, Sudani, Yemen, Italia, Algeria na Misri iliyokaribisha tamasha hilo, kwa lengo la Kurejesha uhai kwao baada ya kupoteza tunzo la vyombo vya habari na utamaduni.
Sherehe ya ufunguzi, ambayo hufanyika kwenye jukwaa la Wizara ya Vijana na Michezo na kuhudhuriwa na Dokta Ashraf Sobhy, itajumuisha maonyesho kutoka nchi zinazoshiriki yanayoonyesha utamaduni wa kila nchi ,kubeba ujumbe wa Amani na Upendo kutoka kwa watoto wa ulimwengu kwa watu wake.
Sherehe ya kufunga tamasha hilo imepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Al-Manara katika (Eltagamoo El Khames ) kwa hudhuria Waziri wa Vijana na Michezo na mawaziri na wahusika muhimu ,Jumapili ijayo.
Tamasha hilo pia litajumuisha maonyesho ya kisanii na Folklore, Vipaji vya kisanaa na uimbaji vinazunguka katika jimbo la Kairo , vituo vya vijana na shule ,Mavazi ya urithi kwa nchi zinazoshiriki, pamoja na semina za wajumbe wote, na mpango wa ziara ya burudani huko Kairo na Giza kuzuru Vivutio vya Watalii ,Tamasha pia linajumuisha ziara za bure kwa timu zinazoshiriki katika maeneo ya urithi na kitamaduni.
Comments