Chini ya Uangalifu wa Rais wa Jamhuri Misri inakaribisha programu kubwa zaidi ya kujitolea ya Kiafrika

Chini ya usimamizi wa Rais Abdel Fattah El Sisi, Wizara ya Vijana na Michezo, kwa kushirikiana na kameshina ya Umoja wa Afrika, zinashikilia Programu ya Kujitolea ya Jumuiya ya Afrika Kundi la 10, Vijana na wasichana 200 kutoka nchi tofauti za Kiafrika, huchaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Bara huko Kairo katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi kutoka 30 Novemba. Mnamo Desemba 12, 2019, katika mfumo wa kuwawezesha kwa kujitolea kwa miezi 12 kama viongozi wa vijana ndani ya vyombo vya Umoja wa kiafrika.

Programu hiyo inakuja ndani ya mfumo wa urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika kwa lengo la kukuza hadhi ya vijana wamisri kama watendaji wakuu katika maendeleo ya bara lao Afrika na kufikia malengo yake, na kuimarisha ushiriki wao ndani ya taasisi za maamuzi za Kiafrika. Programu hiyo pia inachukua jukumu la kubadilishana ujuzi na maarifa ili kujenga bara lenye kufanikiwa na Amani zaidi kwa juhudi za vijana wake.

Programu hiyo inategemea Ajenda ya Afrika 2063 na Mkataba wa Vijana wa Kiafrika kwa uwezeshaji wa vijana kama rasilimali watu wa Kiafrika ambao bara hilo linahangaika kwa kuwaboresha.

Programu ya kujitolea ya AU (AU-YVC) ndio mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika, iliyoanzishwa mnamo 2010 na kukaribishwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika toleo lake la saba kupitia Wizara ya Vijana na Michezo mnamo 2016, na kusifiwa na kameshina ya Umoja wa Afrika kwa uandaaji na utoaji mzuri.

Nchi zinazoshiriki katika tukio hilo ni: Misri - Algeria - Angola - Benin - Burkina Faso - Burundi - Kamerun - Cape Verde - Jamhuri ya Afrika ya Kati - Chad - Kongo - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - Pwani ya Ivory - Djibouti - Guinea ya Ikweta - Ethiopia - Eritrea - Gabon - Ghana - Guinea - Kenya - Liberia - Madagaska - Malawi - Mali - Mauritius - Mauritania - Morocco - Msumbiji - Namibia - Niger - Nigeria - Rwanda - Senegal - Seychelles - Sierra Leone - Somalia - Afrika Kusini - Sudani Kusini - Sudan - Tanzania - Togo Tunisia, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Comoros, Iswatini, Gambia, Lesotho na Sao Tome.

Comments