Wizara ya vijana na michezo hufanyika mahojiano ya awamu ya mwisho ya kukubali wanaojitolea katika programu ya kijitolea katika Umoja wa kiafrika 2019
- 2019-11-21 18:22:54
Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika - idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia ) iliwapokea wamisri wanaofikia awamu ya mwisho kwa kujitolea Programu ya kujitolea ya Umoja wa Afrika 2019, ambapo hatua ya mwisho ilikuwa kwa kufanya mahojiano ya kibinafsi na waombaji wa programu hiyo, na awamu hii ilitangulizwa kwa hatua tatu zilizolenga kuchagua maombi ya Kujiunga kwa programu yaliyokuwa 275.
Mahojiano hayo yalifanywa Jumanne na Jumatano katika makao makuu ya Ofisi ya Vijana ya Afrika katika Wizara ya Vijana na Michezo, na yalifanywa na kamati maalumu ya Wizara ya Vijana na Michezo ili kuwachagua wajitoleaji kulingana na viwango vya Umoja wa Afrika. na mahojiano yanayobaki yataendelea mnamo wiki ijayo ili kujiunga programu hiyo, inayokaribishwa kwa Misri na itakayopangwa kufanyika mjini Kairo kwa wiki mbili, kwenye kituo cha kiolimpiki huko Maadi 2019.
Nchi zinazoshiriki ni pamoja na: Misri - Algeria - Angola - Benin - Burkina Faso - Burundi - Kamerun - Cape Verde - Jamhuri ya Afrika ya Kati - Chad - Kongo - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - Ivory Coast - Djibouti - Guinea ya Ikweta - Ethiopia - Eritrea - Gabon - Ghana - Gine - Kenya - Liberia - Madagaska - Malawi - Mali - Mauritius - Mauritania - Morocco - Msumbiji - Namibia - Niger - Nigeria - Rwanda - Senegal - Shelisheli - Sierra Leone - Somalia - Afrika Kusini - Sudani Kusini - Sudan - Tanzania - Togo - Tunisia - Uganda - Zambia - Zimbabwe - Botswana - Visiwa vya Komoro- Eswatini - Gambia - Lesotho - Sao Tome ".
Ni muhimu kutaja kuwa mpango wa kujitolea wa Umoja wa Afrika mwaka huu unatekelezwa chini ya uangalifu wa Rais wa Jamhuri, Bwana Abdel Fattah El Sisi, sambamba na urais wa Misri wa Umoja wa kiafrika 2019.
Programu hiyo pia inazingatiwa mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika, ulioanzishwa mnamo 2010 na kuukaribishwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika toleo lake la saba kupitia Wizara ya Vijana na Michezo mnamo 2016, na kusifiwa na Tume ya Umoja wa Afrika kwa Upangaji na Utoaji mzuri.
Programu hiyo inalenga kutoa mafunzo kwa vijana waafrika kwa wiki mbili juu ya mada mbali mbali kama itikadi ya Umoja wa Afrika, maendeleo ya ustadi wa uongozi, umahiri na taaluma na ufafanuzi wa Umoja wa Afrika na mambo mengine,na hayo katika mfumo wa kuwawezesha kujitolea kwa miezi 12 kama viongozi vijana ndani ya vyombo vya Umoja wa kiafrika , vinavyoambatana na Ajenda ya Kiafrika ya 2063 na Mkataba wa Vijana wa Kiafrika, ambapo programu inawazingatia vijana ndio watendaji wakuu katika maendeleo na utambuzi wa bara lao la Kiafrika, kuhakikisha malengo yake, na kuimarisha ushiriki wao katika taasisi za maamuzi ya Kiafrika, na huchukua jukumu la kushiriki ujuzi na maarifa kujenga bara lenye ukamilifu. , ufanisi na Amani zaidi lakini kwa juhudi za vijana wake.
Comments