Mmisri Omar Saqr alichukua nafasi ya pili kwenye mashindano ya mpango wa kuharakisha wa wajasiriamali wa Afrika (ANPI)
- 2019-11-22 01:12:33
Dokta.Omar Saqr ,mwanzishi na afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya Nawah ya Kisayansi (Nawah-Scientific),alichukua nafasi ya pili na alipata tuzo lililokadiriwa na Dola elfu 150,katika mashindano ya kwanza ya kila mwaka ya mashindano ya mpango wa kuharakisha wa wajasiriamali wa Afrika (ANPI),yaliyotoa tuzo lilikadiriwa kwa Dola milioni kwa wajasiriamali kumi kutoka nchi mbalimbali za kiafrika. Na karibu wajasiriamali 10,000 wa kiafrika walishiriki katika awamu yake ya kwanza ambapo waliwakilisha nchi 50 za Bara za Afrika.
Mwanzishi wake Jack Ma ambaye ni Bilionea wa kichina,alitangaza mwendelezo wa mashindano hayo ya mpango wa kuharakisha wa wajasiriamali wa Afrika ANPI10 mnamo miaka kadhaa mpaka mwaka wa 2028.
Na pia shirika la AETOS WIRE lilitaja kwamba, taasisi ya Jack Ma ilifanyika wiki hii matukio ya mashindano ya kila mwaka ya kwanza ya mpango wa kuharakisha wa wajasiriamali wa Afrika ANPI.
Jack Ma alianzisha taasisi hiyo baada ya safari yake ya kwanza kwa Afrika mwaka wa 2017, ambayo lengo lake ni kumsaidia na uhamasishaji kizazi kichajo cha wajasiriamali wa Afrika.
Mipango ya kuharakisha kwa wajasiriamali inatoa tuzo lililokadiriwa na Dola milioni kwa wajasiriamali kumi kutoka nchi mbalimbali za Afrika .
Na mpango wa kuharakisha wa wajasiriamali wa Afrika ni ndio kama mpango wa kuharakisha mkuu katika taasisi ya mwajasiriamali wa kichina Jack Ma amabye alianzisha Kikundi cha Ali Baba cha biashara ya kielektroniki.
Matukio ya mwisho ya mashindano hiyo ambayo yaliitwa ( mabingwa wa biashara katika Afrika ) wiki hii mjini Accra ambao ni mji mkuu wa nchi Ghana .
Na wagombea wa juu 10 walionyesha kazi yao kwa kamati ya waamuzi iliyokusanya wataalamu wanne mashuhuri na kwa kuongozwa na Jack Ma, na pia alishiriki katika kamati hiyo Strive Masiwa ambaye ni, mwanzishi na afisi mkuu mtendaji wa kikundi cha Econet.
Comments