Kwa ushirikiano wa vijana wa nchi za Afrika 29 .. Kuzindua shughuli za mkutano wa Afrika kwa kusambaza Amani ya kijamii

Chini ya kauli mbio " tushikamane pamoja " wizara ya vijana na michezo " idara kuu ya ubunge na elimu ya kiraia ilizindua " mkutano wa Afrika " ili kusambaza Amani kwa ushirikiano wa vijana kutoka nchi za Afrika 29 kwenye kituo cha Olimpiki kwenye mtaa wa maadi tangu tarehe 20 mpaka 26 mwezi huu wa Novemba na hivyo chini ya mfumo wa kuzindua kuwa Aswan mjii mkuu wa vijana wa Kiafrika 2019 .
Bibi :- Dina fuaad mwenyekiti wa idara kuu na elimu ya kiraia alisisitiza kuwa wizara ya vijana na michezo ilitekeleza mwaka huu miradi 20 inayohusiana na vijana Waafrika kama ( mkutano wa vijana Waafrika kwa mto wa Nili ) Nili moja .. Mwananchi mmoja, mkutano wa Afrika " tushikamane pamoja " , mkutano wa vijana wa Afrika juu ya " uzalendo na maendeleo " mfano wa uigaji wa umoja wa Afrika " matarajio ya Afrika ... Tamaa Na mustakabali " na anasisitiza kuwa wizara inakaribia kutekeleza miradi sita wakati wa Desemba unaokuja mwaka huo huo na hivyo inakuja pamoja na kutangaza Aswan mji mkuu wa vijana wa Afrika 2019 .

Vilevile , anaashiria umuhimu wa kuelewa vizuri maelezo inayotoa mwito kwa kutowepo ukatili na kutumia njia za Amani zengine ili kusambaza Amani ambapo wizara inaendelea kutekeleza programu " tushikamane pamoja " iliyozindua tangu miaka mitano kwenye kituo cha vijana Kati katika mikoa yote na akiashiria kuwa mwaka huu imesha weka mpango ili kuiwasilisha programu kimataifa kwa lengo la kuongeza uhusiano na vijana wa nchi za Afrika na kutambua utamaduni wa wananchi wao na kupata faida kutoka majaribio yao katika nyanja za ujana mbalimbali .

Vile vile, anafafanua kuwa mkutano unajadili shughuli kadhaa miongoni mwake " maana ya Amani ya kijamii na sehemu zake , jukumu la mwanamke katika kujenga na kuimarisha Amani ya kijamii , kufahimiana na mwengine , Amani ya kijamii katika itikadi ya Kiislamu na kuzuia ukatili , warsha juu ya ushirikiano wa kijamii pamoja na hayo itatekeleza matembezi ya kitalii ili kutazama vivutio muhimu zaidi vya kiutalii vya Misri .
Fuad alionesha kuwa miradi inayohusiana na bara la Afrika inalenga uungaji mkono na kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya nchi za Afrika , kuhamasisha vijana Waafrika , kugundua vipaji vyao ,kuendeleza uzoefu wao na kuwashirikisha katika kutoa maoni yao ili kuendeleza jamii na kuiwasilisha kwa watendaji maamuzi na kuangazia tafauti na utajiri wa utamaduni wa Kiafrika na inayolenga kusambaza maadili ya Amani ya kijamii ili kusimamisha ukatili na itikadi kali .

Comments