"Vijana na Michezo" Ofisi ya Kiafrika hukutana na wahusika wa Umoja wa kiafrika ili kukamilisha hatua za mwisho za mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika

Ofisi ya Vijana ya Kiafrika katika Wizara ya Vijana na Michezo ilikutana na kundi la Kazi la Sekta ya Vijana kwenye kameshina ya Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia katika makao makuu ya kameshina huko Addis Ababa, Ethiopia, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kukaribisha mpango mkubwa zaidi wa kujitolea na Misri ulioandaliwa na kameshina ya Umoja wa kiafrika chini ya uangalifu wa Rais wa Jamhuri, mnamo Novemba na Desemba 2019.

Programu hiyo inakuja ndani ya mfumo wa urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika kwa lengo la kukuza hadhi ya vijana wamisri kama watendaji wakuu katika maendeleo ya bara lao la Afrika na kufikia malengo yake, na kuimarisha ushiriki wao ndani ya taasisi za maamuzi za Kiafrika. Programu hiyo pia inachukua jukumu la kubadilishana ujuzi na maarifa ili kujenga bara lenye ukamilifu zaidi , Ustawi na Amani kwa juhudi za watu wake.

Programu hiyo pia inategemea Ajenda ya Afrika 2063 na mkataba wa Vijana wa Kiafrika kwa suala la kuwawezesha vijana kama rasilimali watu wa Kiafrika ambapo bara kinahangaika kuwakuza.Programu ya Kujitolea ya Umoja wa Afrika (AU-YVC) ndio mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika, ulioanzishwa mnamo mwaka wa 2010 na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri katika toleo lake la saba. Kupitia Wizara ya Vijana na Michezo mnamo 2016, Kameshina ya Umoja wa kiafrika iliisifu kwa upangaji na utoaji mzuri .

Ni muhimu mnamo mwaka huu kutaja kwamba , Misri inawakaribisha vijana na na wasichana 200 kutoka nchi mbali mbali za Kiafrika ili kuhudhuria mafunzo ya Bara huko Kairo kwa siku 15, kama sehemu ya kuwawezesha kwa kujitolea kwa miezi 12 kama viongozi vijana ndani ya vyombo vya Umoja wa kiafrika.

Comments