ujumbe rasmi kutoka wizara ya michezo unawakaribisha mabingwa wa risasi baada ya kushinda kwenye mashindano ya Afrika
- 2019-11-27 14:21:06
Msaidizi wa waziri wa utendaji wa michezo Dokta Mohamed El kordy na kama naibu waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy na msaidizi wa waziri Abd El awal Mohamed walikutana na ujumbe wa timu ya kitaifa ya risasi huko Algeria , hii kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana na ujumbe wa kimisri walioshiriki mashindano ya risasi ya Afrika na kufikia olimpiki ya Tokyo 2020 , mashindano hayo yalifanyika kuanzia Novemba 17 hadi 25 na Misri ilitwaa michuano kwa medali 38 tofauti kutoka medali 19 za dhahabu , 12 za fedha , 7 za shaba
Dokta Ashraf Sobhy alitoa pongezi kwa ujumbe wa kimisri alipongeza utendaji bora uliopatikana na mabingwa hawa na uwezo wa timu ya kimisri kushinda tuzo mbalimbali na tija bora na kuthibitisha ubora na uongozi wa michezo wa kimisri
timu ya Misri ilishinda kwenye mashindano ya pekee medali 8 za dhahabu , 8 za fedha , na 7 za shaba ambapo, wakati wa mashindano ya timu ilishinda medali 11 za dhahabu na 4 za fedha , Tunisia ilikuja kwa pili na medali 8 na Senegal kwa tatu na medali 4
Comments