Waziri msaidizi wa Vijana na Michezo: Uangalifu mkubwa barani Afrika wakati wa enzi ya El-Sisi


Dokta Youssef El Wardani, Waziri Msaidizi wa Vijana na Michezo, alikutana na vijana wa mkutano wa Afrika "tunakamiliana ", uliofanyika katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi kutoka Novemba 20 hadi 26, na kushiriki kwa vijana kutoka nchi 29 za Kiafrika ili kujua mapendekezo ya Mkutano na kuonesha mpango wa vijana na kujadili nao.
Wardani alisisitiza kwamba kuna uangalifu unaokua katika bara la kiafrika wakati wa enzi ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, akisisitiza kuwa: "Wizara ya Vijana na Michezo ilifanya mipango mingi ya jamii na vikao vya mazungumzo na vijana wa nchi za Kiafrika ili kuimarisha mahusiano pamoja na vijana wa bara la Afrika, na hatua hizi hazitasimama mwisho wa urais wa Misri wa Umoja wa Afrika bali huwekwa mihimili ya kiutendaji kwa ajili ya kuiendeleza.


Msaidizi wa Waziri pia alijadiliana na vijana kuhusu maoni ya mipango yao yaliyotoka katika mapendekezo ya Mkutano, ambayo yalifika kwa mipango saba i ikizunguka maswala ya elimu barani Afrika.
Na aliashiria dharura ya kuendeleza mipango hii kwa kushirikiana na washirika husika na kuzitekelezea katika vituo kadhaa vya vijana waliotawanyika katika Jamhuri na hufanya kazi kuunda mtandao wa wakufunzi wa Kiafrika, pamoja na ndugu zao kutoka Misri wanaofanya kazi ili kueneza uelewa wa masuala ya bara kati ya vijana wamisri.

Comments