Waziri wa Vijana na Michezo na Naibu wa Gavana wa Bahari Nyekundu washiriki katika maadhimisho ya Siku ya sherehe ya kutembea huko Hurghada
- 2019-12-01 13:04:13
Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Yousra Attia, Naibu Gavana wa Bahari Nyekundu, na Dokta Emad El Banany, mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo la Misri, Kiarabu na Kiafrika kwa wote walishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutembea iliyoandaliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo, iliyowasilishwa na idara kuu kwa mipango ya maendeleo ya michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la umma la Michezo kwa wote. Sharehe hiyo ilihudhuriwa na washiriki 5,000 huko Hurghada.
Hafla zilianza kutoka
kwa uwanja wa Aquafan kupita katika barabara ya Sheraton kuelekea Marina ya
watalii huko Hurghada.
Maadhimisho hayo inakuja kama sehemu ya mpango wa Olimpiki
ya kwanza ya michezo kwa magavana wa mpaka, uliyofanyika katika mkoa wa Bahari
Nyekundu. Wachezaji 650 waliishirikia kutoka
mikoa ya "Bahari Nyekundu, Aswan, Marsa Matrouh, Alwady Algaded,
Sainai Kusini na Sinai Kaskazini ". mashindano yataendelea hadi
jumatatu ijayo.
Comments