Chini ya Uangalifu wa Rais wa Jamhuri ... Ujumbe mkubwa wa vijana wa Jumuiya ya kiafrika unafika nchini Misri

kupitia mfumo wa ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo (Idara kuu ya Bunge na Elimu ya kiraia - Ofisi ya Vijana ya Afrika) na kameshina ya Umoja wa kiafrika, ujio wa wanaojitolea kwa Jumuiya ya kiafrika ulianza huko Kairo ili kushiriki katika mpango wa kujitolea kwa Umoja wa kiafrika utakaofanyika katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi mnamo 1 hadi 12 Desemba 2019 Chini ya Uangalifu wa Rais Abdel Fattah El Sisi - Rais wa Jamhuri.

Wizara ya Vijana na Michezo ilianza shughuli zake kwa kuwapokea wajumbe waliochaguliwa wa Kiafrika kushiriki katika mpango huu. Hadi sasa, washiriki 160, 20 kutoka Umoja wa Afrika "wakufunzi, waandaaji na waratibu wa programu ndani ya kameshina ya Umoja wa kiafrika na vijana wa kike na kiume wanaojitolea kutoka nchi 32 za kiafrika na wajitolea 20 kutoka Misri.


Timu ya wataalamu wa kameshina ya Umoja wa kiafrika pamoja na Ofisi ya Vijana ya Afrika hukamilisha maandalizi yao ya kuanza mafunzo yaliyopangwa kuzinduliwa Jumapili, na baada ya kukamilika kwa mkutano wa maandalizi ya mwisho kwa mpango huo na uandaaji wa majukumu na shughuli zote, kwa pamoja walitembelea kuangalia vyumba vya mafunzo na semina kwa ajili ya kutoa programu hiyo kwa njia bora kama inavyowezekana.

Inatajwa kwamba Programu ya kujitolea ya AU (AU-YVC) ndio mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani Afrika, uliozinduliwa mnamo 2010. unaofanya kazi sambamba na Agenda ya Umoja wa kiafrika 2063, na unalenga kuwawezesha vijana ili kuwaajiriwa katika nyanja za maendeleo ili kuhudumia nchi zote za Kiafrika katika Sekta kadhaa na taasisi tofauti.

Comments