UNESCO inatangaza ushindi wa "Aswan" kwa tuzo ya miji 10 bora zaidi ya kujifunza ulimwenguni

Gavana wa zamani wa Aswan  Bwana Ahmed Ibrahim alipokea Tuzo la Dunia, baada ya kuuchagua Aswan kama moja wapo ya miji 10 bora zaidi ya kujifunza kwa mwaka wa 2019, Wakati wa sherehe rasmi kwa Mkutano wa kila mwaka wa Kimataifa kwa Mtandao wa Miji ya Kujifunza (GNLC), Imeandaliwa na Taasisi ya UNESCO ya Kujifunza Maisha Yote (UIL) ya UNESCO huko Medellin, Colombia.


Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Rais wa Colombia Ivan Duque na Dokta. Malak Zaalouk, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kujifunza ya Mashariki ya Kati,  Balozi Sami Salem, Balozi wa Misri kwenda Colombia, na Federico Gutierrez, Meya wa Medellin,Na pia washiriki wa Mtandao wa Miji ya Kujifunza na wakilishi kutoka nchi 159 ulimwenguni, Mervat Elsamman ana jukumu la mawasiliano, Kwa kuongeza idadi kubwa ya wakilishi wa mashirika ya UN,Asasi za kikanda, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na mashirika ya kimataifa.


Gavana wa zamani wa Aswan alipokea Tuzo la Mtandao wa Miji ya Kujifunza baada ya ushindi wa 

 Aswan kati ya miji 10 bora zaidi ulimwenguni, inayopewa na Taasisi ya UNESCO ya Kujifunza maisha yote, ikifuatiwa na shirika la kimataifa la UNESCO.


Dokta  Ghada Abdel Bari, Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya UNESCO nchini Misri, alisema ,Kulingana na Ofisi ya Habari ya Umoja wa Mataifa, kuwa mradi wa Miji ya Kujifunza ya UNESCO unalenga elimu kwa vijana na wazee katika kila mji, Katika Kamati ya Kitaifa tulifanya kazi na miji ya Aswan na Giza, na Aswan ilijiunga na miji ya kujifunzia kwa idhini ya nchi zote wanachama, Aswan ilishinda tuzo ya Jiji la Kujifunza la 2019 kwa Malengo ya  Maendeleo endelevu , Hasa, lengo la nne la elimu kamili na bora,  inayofanikisha usawa kati ya wanaume na wanawake, inaambatana na Ajenda ya 2030 ya maendeleo ya Misri, hasa katika nyanja za elimu na elimu ya juu.


Mervat El Samman, mratibu wa miji la Aswan kwa miji ya kujifunza ya UNESCO aliashiria kuwa ushindani huo ulihudhuriwa na zaidi ya nchi 150  zinazowakilisha washiriki wa Mtandao  wa kimataifa wa UNESCO wa Miji ya Kujifunza kushindana miji bora  iliyopata maendeleo katika elimu na ujifunzaji.


Na aliongeza kuwa " Aswan alikuwa mwanachama wa Miji ya Kujifunza ya UNESCO mnamo 2017, Hii ilikuwa moja wapo ya masharti ya kuomba Tuzo ya Miji ya Kujifunza, kwa hivyo tukaandaa faili yenye thamani sana inayostahili jina la Aswan na Misiri,Kwa msaada wa kamati ya Kitaifa ya UNESCO, tuliwasilisha faili iliyo na shughuli za shule, kijitabu cha Aswan na kinachotofautisha, Na mafanikio kwenye msingi sio katika elimu tu bali pia katika kujifunza. "


Mkoa wa Aswan una shule 20 zipatazo  zinazotumia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.


Uteuzi wa mji wa Aswan kati ya miji 10 bora zaidi kwa kujifunza ya 2019 na UNESCO, ni mafanikio ya kushangaza kwa Kukuza ufundishaji na ujifunzaji kupitia sera na mipango ubunifu na malengo maalum na kukuza mkakati wa kuchanganya na kubadilisha miradi, Hii ni pamoja na mipango ya uhifadhi wa bustani na maji katika shule, na pia kutoa fursa tofauti za mafunzo kwa miradi ya sehemu zote za jamii.

Comments