Kwa ushirikiano pamoja na Al-Azhar, kozi za kwanza za lugha ya Kiarabu zilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Burundi


DKt Abeer Bassiouni, Balozi wa Misri nchini Burundi, alisema kuwa kozi za lugha za Kiarabu zilianzishwa kwa mara ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Burundi kupitia kituo cha kufundisha Lugha kwenye chuo kikuu , Kozi zinaanza na wanafunzi 60 waburundi kama hatua ya kwanza, imegawanywa kwa vikundi vitatu (kila kikundi cha wanafunzi 20) masheikh wa Al-Azhar waliotumwa Burundi watafundisha kozi hizi, Shughuli hizi zinakuja kulingana na  ushirikiano wa kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili na mchango mkuu wa  Al-Azhar katika suala hili.


Ikumbukwe kwamba wajumbe wa Al-Azhar Al-Sharif wanafanya shughuli nyingi za kijamii na kiutamaduni na  -kwa kujitolea- wamefanya kozi za bure kwa wale wanaopenda kujifunza Kiarabu,

  Na mnamo miaka mitatu iliyopita, Ubalozi umefanikiwa kuingiza kujifunza lugha ya Kiarabu katika misikiti, Chuo Kikuu cha Salaam ,au Chuo Kikuu cha Bujumbura sasa, pamoja na kazi ya msingi ya Wasomi wa Al Azhar al-Sharif  wa kufundisha katika Shule ya Al-Tahdheeb ya Kiislamu.

Comments