Kwa mara ya kwanza, na kwa mahudhurio ya nchi zote za Afrika, Wizara ya Vijana na Michezo hufungua programu ya kumi kwa wanaojitolea wa wa Umoja wa kiafrika

Wizara ya Vijana na Michezo (Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia- Ofisi ya Vijana waafrika) ilianzisha matukio ya Programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika kwa kushirikiana na Kameshina ya Umoja wa kiafrika mnamo kipindi cha Novemba 28 hadi Desemba 13 mwaka wa 2019.

Na Rais Elsisi anazingatiwa Rais wa nchi moja wa kwanza anayejali tukio hilo kwa njia rasmi tangu uanzishi wake katika 2010, nalo linalosisitiza shime ya uongozi wa kisiasa wa kimisri na usaidizi wake usio na mipaka kwa shughuli za vijana waafrika barani.

Na Mheshemiwa Rais Abd El Fatah El Sisi -Rais wa Jamhuri ya Misri ya kiarabu- wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika, ameangalia mipango na programu kadhaa zinazolenga kuwasaidia vijana waafrika na kuwawezesha katika nyanja tofauti, na Urais wa Misri unahitimiwa kwa kuipokea programu kubwa zaidi barani kwa wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika.

Sherehe hiyo ilijumuisha kauli ya Bibi Dina Fouad "Mwakilishi wa Wizara na Rais wa Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia akiwakilisha Wizara ya Vijana na Michezo " na Bibi Brodenis "Mjumbe wa Kameshina wa Umoja wa kiafrika, akiiwakilisha" na Bibi Dina Fouad alianza kauli yake akimwashiria Mheshemiwa Waziri wa Vijana na Michezo Profesa Ashraf Sobhy, na kuyapeleka mapongezi yake kwa mahudhurio na wanaojitolea, naye mnamo kauli yake alizungumzia programu muhimu zaidi zinazohusu bara la kiafrika zilizoteklezwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo mnamo Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika.Na Bibi Brodenis alianza kauli yake kwa kuwakaribisha wanaohudhuria na kuishukuru Misri kwa wema na uzuri wa kuwakaribisha wote, na alitumika nafasi ya kauli yake ili kumshukuru Bwana Hassan Ghazali "Mratibu mkuu wa Ofisi ya Vijana waafrika kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, na Naibu wa Rais wa Umoja wa kiafrika, akipeleka mapokezi kwa timu yake, akiashiria kwamba yeye ni kijana mwafrika kiongozi , akifanya utani kwa kusema kwamba yeye ni mtu mwenye harakati nyingi na anayapenda matatizo lakini hayaogopi, pia daima hutia masuluhisho yanayofaa, pia akiashiria uzalendo wake kwa Umoja wa kiafrika, na alimshukuru tena kwa juhudi na hamasa zake, kisha alielekea kwa kusifu historia ya kutekleza programu ya wanaojitolea wa Umoja wa kiafrika, na mahali pa kuyakaribisha makundi yaliyopita, akiashiria kuikaribisha kwenye Misri mwaka wa 2016 na furaha yake kwa kuirudia tena katika Kundi la kumi.

Pia alielezea Haja ya Umoja wa kiafrika kwa kuwachagua wanachama watendaji katika kundi hili na kuwepo nafasi za kazi zinazowangoja, pia haja ya Umoja wa kiafrika kwa juhudi zao, pamoja na kuwepo mkusanyiko wa wataalamu unaohusu ajira na kuwafuatilia kwa wanafunzi wote na kuwatathmini kulingana na viwango vya Umoja wa kiafrika.

Na umuhimu wa Mapokezi ya Misri kwa programu hiyo upo kwamba jaribio la kuishiana pamoja na vijana kutoka nchi tofauti za kiafrika, linaloimarisha kubadilishana utamaduni, maoni, na mawazo kati ya viongozi vijana waafrika. Pia inawezekana kwa vijana waafrika kujua zaidi kuhusu nchi ya kimisri na mafanikio yake. Na mafanikio ya jaribio la kimisri yanaonekana katika suala la kuwawezesha vijana na huongezeka kuwa jaribio kuu la kikanda kupitia vijana wamisri.

Comments