Uainishaji wa Skwashi.. Ranem kwa mwaka mmoja kwenye juu.. Alsherbeeny anapata nafasi ya pili na Hanya baina ya mabingwa
- 2019-12-04 10:29:24
Chama cha wachezaji wa Skwashi wanaocheza nje (PSA) kimetangazia uainishaji mpya wa kidunia wa wanawake mnamo mwezi wa Desemba, bingwa Mmisri Ranem Alwalily ambaye ni mchezaji wa klabu ya Wadi Degla amehifadhi nafasi yake ya kwanza ya uainishaji wa kidunia kwa mwezi wa 12 mfululizo, tangu amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Nour Alsherbeeny mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa Desemba, mwaka uliopita.
Nour Alsherbeeny amerudia nafasi yake ya pili katika uainishaji wa kidunia baada ya kuchukua nafasi ya nne katika uainishaji wa mwezi wa Novemba, hii baada ya ufuzu wa bingwa Mmisri kwa michuano ya wanawake ya dunia hivi karibuni na iliyofanyika chini ya miguu ya piramidi, mwezi wa Novemba uliopita.
Katika nafasi ya tatu, mchezaji wa klabu ya Wadi Degla Noran Gohar amerudi hadi nafasi hiyo na ambaye amefika nusu ya fainali ya michuano ya wanawake ya dunia, kabla ya kuondoka kwake kutoka michuano hiyo dhidi ya mwenzake wa klabu ya Wadi Degla (Ranem Alwalily), na katika uainishaji wa nne, mchezaji wa klabu ya Heliopolis amerudi baada ya kujiondoa kwake kutoka robo ya fainali ya michuano ya dunia.
Orodha ya wachezaji 10 wa kwanza imeshuhudia tukio jipya, baada ya Misri imeweza kuchukua nafasi nne za kwanza katika uainishaji, bingwa Mmisri (Hanya Alhamamy) imeweza kuingiza orodha ya wachezaji 10 wa kwanza kwenye kiwango cha ulimwengu ili kuchukua nafasi ya kumi katika uainishaji baada ya kufika kwake nusu ya fainali ya michuano ya wanawake ya dunia, ambapo ameshindwa dhidi ya Nour Alsherbeeny ambaye ameshinda michuano hiyo kwa mara ya nne katika historia yake.
Comments