Dkt "Mustafa Madbouly" Waziri Mkuu alikutana na Dkt. Khaled Abdel Ghaffar Waziri wa Elimu ya Juu, Dkt. Hany Helal Rais wa Chuo Kikuu Senghor, Jumanne,7/5/2019.
Mshauri "Nader Saad" Msemaji wa baraza la mawaziri alisema kuwa mnamo mkutano huo zilionyeshwa shughuli za Chuo Kikuu huko Misri tangu ufunguzi wake mwaka 1990 , ambapo Idadi ya wahitimu tangu kuanzishwa chuo kikuu imefikia wahitimu 2592, na maiongoni mwao wahitimu 1844 kutoka makao ya chuo kikuu huko Aleskandaria, na wahitimu 748 kutoka sehemu za Chuo Kikuu cha Sangour katika nchi za Afrika.
Chuo Kikuu kina lengo la kuimarisha maendeleo barani Afrika kwa njia ya Kufundisha waanzishi wa maamuzi ndani ya sekta za kiserikali na za binafsi, wanaopata kutoka chuo kikuu shahada ya Uzamili katika maendeleo, shahada Iliyothibitishwa kwa Umoja wa Ulaya na Baraza Kuu la Vyuo vikuu vya kimisri, Wakati wa mkutano huo, Dkt Hani Hilal aliomba kutoa makao ya kudumu kwa Chuo Kikuu badala ya ghorofa tano ambayo sasa inashikilia mnara wa Kotton huko Aleksandria , Ambapo kuna ruhusa ya awali ya kutenga ardhi ya mita za mraba 5000, kwa ujenzi wa majengo ya elimu na makazi kwa wanafunzi katika mahali pamoja, Hilal aliomba kuingilia kwa Waziri Mkuu ili kuharakisha ruhusa ya ugawaji ili kuweza kuanza ujenzi.
Msemaji wa Baraza la Mawaziri aliongeza kuwa Dkt. Mustafa Madbouli alisifu mchango wa Chuo Kikuu cha Sengour wa kuyaimerisha maendeleo na kupatikana uwezo barani Afrika , pia Wakati wa mkutano huo, Waziri Mkuu aliwasiliana na Gavana wa Mkoa wa Aleksandria , Aliongoza haraka ya shughuli kuchakua hatua muhimu na kuratibu pamoja na idara ya Chuo Kikuu cha Sungor kuhusu ardhi inayohitajika kwa makao ya Chuo Kikuu.
Comments