Kupambana Umaskini, kukuza Maendeleo na Ujenzi mpya barani Afrika... Rais: tunashirikiana pamoja na "NEPAD" na Frankfonia ili kuhakikisha matarjio ya nchi za bara


Rais Abd Elfatah Elsisi alisisitiza kwba Misri inaangalia sana kuunga mkono Wakala ya Umoja wa kiafrika kwa maendeleo "NEPAD", kupitia kuimarisha mikakati na mipango yake ili kuchangia kuboresha Afrika, na kuzidisha Ushirikiano na ukamilifu kati ya nchi zake, ili kupambana na matatizo ya bara kama Umaskini, na kupunguza viwango vya maendeleo. 


Jana mnamo kupokeza Dokta Ibrahim Mayaky" mkurugenzi mtendaji wa NEPAD" kwa mahudhurio ya Sameh Shokry " Waziri wa mambo ya nje" Rais ameashiria kwamba Misri ni  nchi moja ya zilizoanzisha wakala hii na inaangalia kuendelea mfululizo wa mafanikio ulioanzishwa kwa wakala. 


Na Balozi Bassam Rady " Msemaji wa Urais" alieleza kwamba mkutano ulishuhudia mwafaka wa kuongeza Ushirikiano kati ya pande mbili, ili kuunga mkono mipango ya wakala hii yanayolenga kuboresha Ukamilifu wa kiuchumi na unganisho wa kikanda barani Afrika, khasa miradi ya Miundombinu yenye jicho la kibara, ambayo inazingatiwa kipaumbele cha kwanza cha Misri mnamo Urais wake wa umoja wa kiafrika, na akiashiria kwa kuhangaika ili kutimiza miradi ya kinjia cha kaskazini- kusini " njia ya Kairo- Cape town ", na kuunganisha kwa Ubaharia kati ya bahari ya kati na ziwa la Victoria.


Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa NEPAD, alisifu mchango mwongozi wa kimisri katika kutekleza Programu za maendeleo y kijamii na kiuchumi barani Afrika, ambao unawakilishwa katika Ushirikiano wake wa kuzindua mpango wa NEPAD mpaka uwe  chombo kikuu cha kiafrika ili kuonyesha changamoto za kimaendeleo barani kwa upande wa kiafrika na kimataifa. 


Bwana "Mayaky" alieleza kwamba anaangalia utaratibu endelevu na Misri ili kufikia kwao jaribio lake kubwa kwenye uteklezaji miradi na Programu kwa mpango, kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo endelevu barani, pia kufaidika kutoka uzoefu wa kimisri wa kuandaa makada waafrika katika nyanja zote, khasa Afya, Kilimo, na Nishati pamoja na kushirikiana na Misri ili kusanya Fedha toka washiriki na kuzielekea miradi ya upande wa kiafrika, pia inayotajwa kwenye Ajenda ya maendeleo ya kiafrika 2063.


Kutokana na upande mwingine Rais Elsisi amesisitiza kwamba Kairo inaangalia kuzidisha Ushirikiano pamoja na shirikisho la kifaransa"Francophone",ili kuchukua mchango wake wa kuhakikisha matarajio ya wananchi wa nchi zinazoendelea, akieleza kukaribishwa kwake kwa Ushirikiano wa pande tatu pamoja na shirika, ili kuunga mkono wa nchi za kiafrika, khasa Kuangalia Vijana, Wanawake, Ujasiriamali, Kupambana na Ugaidi, na Fikiria Kali. 


Hayo yote yalitokea jana mnamo mapokezi ya Elsisi kwa bibi "Louise Moschikwabo" " Katibu mkuu wa shirikisho la kifaransa, kwa kuhudhuria bwana Sameh Shokry " Waziri wa mambo ya nje". 


Na Balozi Bassam Rady ameeleza kwamba Rais alionyesha kwamba Misri ipo tayari ya kutoa uzoefu unaolazimishwa kwa shirikisho ili kuhakikisha malengo yake, wakati wa kuimarisha njia za Ushirikiano kati ya Misri na maeneo ya kiafrika yanayotamka kifaransa. 


Na bwana Rady alieleza kwamba Katibu mkuu wa kifaransa ametoa shukuru kwa Misri kwa Usaidizi wake wa kihistoria kwa shirikisho, na ameonyesha mchango mkuu wa Misri sawa upo kwenye uwanja wa kikanda au kwenye shirikisho kwa ujumla, na " Louise Moschikwabo" amesifu Usaidizi wa Misri kwa chuo kikuu cha "Singur" katika Aleksandria, kama ni kimoja cha taasisi za kielimu na kiutamaduni kwa shirikisho hilo, akionyesha kwamba shirikisho linatoa juhudi za kuboresha chuo Kikuu ili kiwe kituo cha ubunifu wa kisayansi. 


Na mkutano ulielekea kwa umuhimu wa maendeleo ya shirikisho kuzisaidia nchi wanachama zenye migogoro, pamoja na Uandaaji wa Misri ili kutoa msaada kwa nchi ili zapita changamoto zinazozikabiliana, mnamo wakati wa mchango wa Misri kwa kupatikana Amani barani Afrika, ambao huchukua nafasi kubwa mnamo Urais wake wa hivi sasa kwa Umoja wa kiafrika, pia uamuzi wa kilele cha kiafrika cha mwisho kwa kutoa uongozi wa Folda za ujenzi mpya na maendeleo baada ya migogoro kwa Rais Elsisi.

Comments